Kikunda

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Kikunda ni lugha ya Kibantu nchini Zimbabwe na Zambia inayozungumzwa na Wakunda. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kikunda nchini Zimbabwe imehesabiwa kuwa watu 145,000, na nchini Zambia watu 43,800. Pia kuna wasemaji 5500 nchini Msumbiji. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kikunda kiko katika kundi la N40.

Viungo vya nje [hariri]

Viambishi ni mofimu au viungo vyenye maana ambavyo hufungamanishwa na mzizi/shina la neno ili kulipa neno hilo maana mbalimbali za kisarufi kama vile nafsi, wakati, hali, urejeshi, n.k Viambishi awali ni vile vinavyotangulia mzizi wenyewe, yaani huwa kabla ya mzizi/shina. SHINA AU MZIZI: Hakuna tofauti kati ya shina na mzizi MZIZI/SHINA, Ni sehemu ya neno inayobeba maana yake kuu na huwa haibadiliki, Kwa mfano, tuangalie vitenzi vifuatavyo: a-na-LIM-a wa-li-LIM-i-a ni-ta-LIM-iw-a wa-na-vyo-LIM-a Ukiangalia kwa makini, utaona kuna sehemu ya kitenzi hiki ambayo haibadiliki katika mifano ya hapo juu. Sehemu hiyo ni (-LIM-). Na hii ndiyo shina au mzizi wa kitenzi LIMA. Mfano mwingine: a-li-ki-SOM-a hu-SOM-ew-a wa-li-SOM-e-an-a a-li-m-SOM-e-a i-li-SOM-w-a Tunaona hapa mzizi/shina la kitenzi SOMA, ni -som- Ili utambue shina/mzizi wa kitenzi unafaa kuwazia hali mbalimbali au kauli tofautitofauti za mnyambuliko wa kitenzi halafu ubainishe sehemu isiyobadilika.