Kikuche
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Kikuche | ||||||||||||||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kikuche utosi-mweusi
|
||||||||||||||||||
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
|
Vikuche ni ndege wakubwa kiasi wa jenasi Tchagra katika familia Malaconotidae. Wanatokea Afrika kusini kwa Sahara tu. Ndege hawa wana rangi ya kijivu mgongoni, rangi ya kahawiachekundu mbawani na rangi ya kijivu au nyeupe chini; mlia mweusi unapitia macho. Wana domo nene lenye ncha kwa kulabu. Hula wadudu wakubwa hasa na vertebrata wadogo pia, kama vyura, mijusi na nyoka wadogo. Hulijenga tago lao kwa umbo wa kikombe mtini au kichakani na jike huyataga mayai 2-3.
Spishi [hariri]
- Tchagra australis, Kikuche Mwakijo (Brown-crowned Tchagra)
- Tchagra anchietae, Kikuche wa Anchieta (Anchieta's Tchagra)
- Tchagra jamesi, Kikuche Michirizi-mitatu (Three-streaked Tchagra)
- Tchagra minutus, Kikuche Mdogo (Marsh Tchagra) - inaainishwa pia katika Bocagia
- Tchagra senegalus, Kikuche Utosi-mweusi (Black-crowned Tchagra)
- Tchagra tchagra, Kikuche Kusi (Southern Tchagra)