Kikucha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kikucha
Kikucha domo-refu
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Sylvioidea (Ndege kama kucha)
Familia: Macrosphenidae (Ndege walio na mnasaba na kolojojo)
Jenasi: Sylvietta
Lafresnaye, 1839
Ngazi za chini

Spishi 9:

Vikucha au vibubutu ni ndege wadogo ambao zamani waliainishwa katika Sylviidae, familia ya kucha wengine. Sasa wataalamu wanakubaliana kwamba labda ndege hawa ni kundi lao lenyewe pamoja na kolojojo na spishi nyingine za kucha wa Afrika. Kwa sasa hakuna uhakika kama ndege hawa wote waunda familia yao au wamo katika familia mbalimbali. Wanafanana na shoro, kuchanyika na kuchamsitu ambao zamani waliainishwa pia katika familia Sylviidae. Vikucha ni wadogo zaidi na wana mkia mfupi sana. Rangi zao ni kahawia na nyekundu, kijani au njano. Hula wadudu ambao huwatafuta ardhini au kwa mashina na matawi ya miti. Hulijenga tago lao kwa umbo wa kikapu kwa manyasi, tandabui na nyuzinyuzi za mimea chini ya tawi la chini la mti. Jike huyataga mayai 1-3.

Spishi za Afrika[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]