Kihorogota

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kihorogota ni kata ya tarafa ya Ismani, Wilaya ya Iringa Vijijini, katika Mkoa wa Iringa, Tanzania, yenye Postikodi namba 51210.

Katika sensa iliyofanyika mwaka 2022 wakazi walihesabika kuwa 8,899 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 7,688 waishio humo. [2]

Upande wa dini, wengi ni Wakristo, hasa wa Kanisa Katoliki, lakini pia Walutheri.

Ni eneo maarufu kwa kilimo hasa cha mahindi, ingawa ardhi imechoka kutokana na matumizi makubwa, hasa katika miaka ya 1950 na 1960, Ismani peke yake ilipokuwa inaweza kuzalisha kuliko Tanzania nzima.

Siku hizi barabara inayopita kijijini ikiunganisha Iringa na Dodoma, hivyo pia Cape Town na Kairo, imetiwa lami.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Kata za Wilaya ya Iringa Vijijini - Tanzania

Idodi | Ifunda | Ilolompya | Itunundu | Izazi | Kalenga | Kihanga | Kihorogota | Kising'a | Kiwere | Luhota | Lumuli | Lyamgungwe | Maboga | Magulilwa | Mahuninga | Malengamakali | Masaka | Mboliboli | Mgama | Migoli | Mlenge | Mlowa | Mseke | Nyang'oro | Nzihi | Ulanda | Wasa


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Iringa bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kihorogota kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.