Kiguudau
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Kiguudau | ||||||||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
|
Viguudau ni ndege wa maji wa familia Heliornithidae. Familia hii ina spishi tatu tu, kila moja katika jenasi yake. Ndege hawa wana mwili mwembamba, shingo refu, mkia mpana na domo lenye ncha kali. Wana tando za ngozi kati ya vidole vyao zinazowasaidia kuogelea. Wanatokea kanda za tropiki kwa maji yatiririkayo polepole au katika vinamasi na mabwawa ya mikoko. Hula wadudu, makoa, gegereka, vyura na samaki wadogo. Hujenga tago lao la vitawi na mimea kwa matete.
[hariri] Spishi ya Afrika
- Podica senegalensis, Kiguudau wa Afrika (African Finfoot)
[hariri] Spishi za mabara mengine
- Heliopais personata (Masked Finfoot)
- Heliornis fulica (Sungrebe)