Kigong'ota
| Kigong'ota | ||||||||||||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Vigong'ota, gongonola, gogota, vigotagota au ving'ota ni ndege wa nusufamilia Picinae katika familia Picidae. Ni bora kutengea spishi za nusufamilia Picumninae jina “kigogota”. Inawakilishwa katika Afrika na kigogota wa Afrika. Vigong'ota vinatokea misituni na maeneo mengine yenye miti kila mahali pa dunia isipokuwa Madagaska, Australia, New Zealand na kanda za Aktiki na Antaktiki.
Spishi nyingi ni nyeusi mgongoni kwenye madoa na/au mabaka meupe au njano. Spishi nyingine zina rangi ya majani au kahawa. Miguu yao ina vidole viwili vikabilivyo mbele na viwili vikabilivyo nyuma. Mkia una manyoya shupavu na umsaidia ndege kutembea wima mashinani kwa miti. Ndege hawa wana domo lenye nguvu ambalo hutumia kugogota miti na kutafuta wadudu katika nyufa za miti. Ulimi wao mrefu wa kunata na wenye nywele uwasaidia kuwatoa wadudu. Zaidi ya wadudu vigong'ota hula matunda na makokwa; spishi nyingine hula hata utomvu wa miti. Dume huchimba tundu katika mti na pengine jike amsaidia. Huyu huyataga mayai 2-6 ndani ya tundu.
Spishi za Afrika [hariri]
- Campethera abingoni, Kigong'ota Mkia-njano Golden-tailed Woodpecker)
- Campethera bennettii, Kigong'ota Sharubu-jekundu (Bennett's Woodpecker)
- Campethera cailliautii, Kigong'ota Mgongo-kijani (Green-backed Woodpecker)
- Campethera caroli, Kigong'ota Masikio-kahawia (Brown-eared Woodpecker)
- Campethera maculosa, Kigong'ota Miraba (Little Green Woodpecker)
- Campethera mombassica, Kigong'ota wa Mombasa (Mombasa Woodpecker)
- Campethera nivosa, Kigong'ota Kisogo-chekundu (Buff-spotted Woodpecker)
- Campethera notata, Kigong'ota wa Knysna (Knysna Woodpecker)
- Campethera nubica, Kigong'ota Nubi (Nubian Woodpecker)
- Campethera punctuligera, Kigong'ota Madoa-madogo (Fine-spotted Woodpecker)
- Campethera scriptoricauda, Kigong'ota Kipaku Speckle-throated au Reichenow's Woodpecker)
- Campethera tullbergi, Kigong'ota Miraba au Gongonola (Tullberg's Woodpecker)
- Dendrocopos major, Kigong'ota Madoa-meupe Mkubwa (Great Spotted Woodpecker)
- Dendrocopos minor, Kigong'ota Madoa-meupe Mdogo (Lesser Spotted Woodpecker)
- Dendropicos abyssinicus, Kigong'ota Habeshi (Abyssinian Woodpecker)
- Dendropicos elachus, Kigong'ota Kijivu Mdogo (Little Grey Woodpecker)
- Dendropicos elliotii, Kigong'ota wa Elliot (Elliot's Woodpecker)
- Dendropicos fuscescens, Kigong'ota Mgongo-miraba (Cardinal Woodpecker)
- Dendropicos gabonensis, Kigong'ota wa Gabon (Gabon Woodpecker)
- Dendropicos goertae, Kigong'ota Kijivu (African Grey Woodpecker)
- Dendropicos griseocephalus, Kigong'ota Kijanikijivu (Olive Woodpecker)
- Dendropicos lugubris, Kigong'ota Huzuni (Melancholy Woodpecker)
- Dendropicos namaquus, Kigong'ota Kidevu-cheusi (Bearded Woodpecker)
- Dendropicos obsoletus, Kigong'ota Mgongo-mwekundu Brown-backed Woodpecker)
- Dendropicos poecilolaemus, Kigong'ota Kidari-madoa (Speckle-breasted Woodpecker)
- Dendropicos pyrrhogaster, Kigong'ota Tumbo-jekundu (Fire-bellied Woodpecker)
- Dendropicos spodocephalus, Kigong'ota Kichwa-kijivu (Eastern Grey Woodpecker)
- Dendropicos stierlingi, Kigong'ota-miyombo (Stierling's Woodpecker)
- Dendropicos xantholophus, Kigong'ota Kishungi-njano (Yellow-crested Woodpecker)
- Geocolaptes olivaceus, Kigong'ota-ardhi (Ground Woodpecker)
- Picus vaillantii, Kigong'ota Kijani wa Afrika (Levaillant's Woodpecker)
Jenasi za mabara mengine [hariri]
- Blythipicus (spishi 2)
- Campephilus (spishi 11)
- Celeus (spishi 11)
- Chrysocolaptes (spishi 8)
- Chrysophlegma (spishi 3)
- Colaptes (spishi 13)
- Dendrocopos (spishi 24)
- Dinopium (spishi 4)
- Dryocopus (spishi 7)
- Gecinulus (spishi 2)
- Hemicircus (spishi 2)
- Meiglyptes (spishi 3)
- Melanerpes (spishi 24)
- Micropternus (spishi 1: Rufous Woodpecker)
- Mulleripicus (spishi 3)
- Picoides (spishi 12)
- Piculus (spishi 7)
- Picus (spishi 12)
- Reinwardtipicus (spishi 1: Orange-backed Woodpecker)
- Sapheopipo (spishi 1: Okinawa Woodpecker)
- Sphyrapicus (spishi 4)
- Veniliornis (spishi 14)
- Xiphidiopicus (spishi 1: Cuban Green Woodpecker)