Kigbaya-Kaskazini
Kigbaya-Kaskazini ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati na Kamerun inayozungumzwa na Wagbaya. Mwaka wa 1996 idadi ya wasemaji wa Kigbaya-Kaskazini nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati imehesabiwa kuwa watu 200,000; na mwaka wa 1980 idadi ya wasemaji nchini Kamerun imehesabiwa kuwa watu 72,500. Pia kuna wasemaji wachache nchini Jamhuri ya Kongo na Nigeria. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kigbaya-Kaskazini kiko katika kundi la Kiadamawa-Ubangi.
Viungo vya nje [hariri]
- lugha ya Kigbaya-Kaskazini kwenye Multitree
- ramani ya Kigbaya-Kaskazini
- http://www.ethnologue.org/show_language.asp?code=gya
Viambishi ni mofimu au viungo vyenye maana ambavyo hufungamanishwa na mzizi/shina la neno ili kulipa neno hilo maana mbalimbali za kisarufi kama vile nafsi, wakati, hali, urejeshi, n.k Viambishi awali ni vile vinavyotangulia mzizi wenyewe, yaani huwa kabla ya mzizi/shina. SHINA AU MZIZI: Hakuna tofauti kati ya shina na mzizi MZIZI/SHINA, Ni sehemu ya neno inayobeba maana yake kuu na huwa haibadiliki, Kwa mfano, tuangalie vitenzi vifuatavyo: a-na-LIM-a wa-li-LIM-i-a ni-ta-LIM-iw-a wa-na-vyo-LIM-a Ukiangalia kwa makini, utaona kuna sehemu ya kitenzi hiki ambayo haibadiliki katika mifano ya hapo juu. Sehemu hiyo ni (-LIM-). Na hii ndiyo shina au mzizi wa kitenzi LIMA. Mfano mwingine: a-li-ki-SOM-a hu-SOM-ew-a wa-li-SOM-e-an-a a-li-m-SOM-e-a i-li-SOM-w-a Tunaona hapa mzizi/shina la kitenzi SOMA, ni -som- Ili utambue shina/mzizi wa kitenzi unafaa kuwazia hali mbalimbali au kauli tofautitofauti za mnyambuliko wa kitenzi halafu ubainishe sehemu isiyobadilika.