Kifulfulde-Adamawa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Kifulfulde-Adamawa ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Kamerun, Chad na Sudani inayozungumzwa na Wafulfulde. Lugha hiyo ni lugha mojawapo ya lugha za Kifulfulde. Mwaka wa 1986 idadi ya wasemaji wa Kifulfulde-Adamawa imehesabiwa kuwa watu 669,000 nchini Kamerun. Mwaka wa 1982 idadi ya wasemaji wa Kifulfulde-Adamawa imehesabiwa kuwa watu 90,000 nchini Sudani. Mwaka wa 2006 idadi ya wasemaji wa Kifulfulde-Adamawa imehesabiwa kuwa watu 148,000 nchini Chad. Pia kuna wasemaji nchini Nigeria na Marekani. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kifulfulde-Adamawa kiko katika kundi la Kiatlantiki.

Viungo vya nje [hariri]

Viambishi ni mofimu au viungo vyenye maana ambavyo hufungamanishwa na mzizi/shina la neno ili kulipa neno hilo maana mbalimbali za kisarufi kama vile nafsi, wakati, hali, urejeshi, n.k Viambishi awali ni vile vinavyotangulia mzizi wenyewe, yaani huwa kabla ya mzizi/shina. SHINA AU MZIZI: Hakuna tofauti kati ya shina na mzizi MZIZI/SHINA, Ni sehemu ya neno inayobeba maana yake kuu na huwa haibadiliki, Kwa mfano, tuangalie vitenzi vifuatavyo: a-na-LIM-a wa-li-LIM-i-a ni-ta-LIM-iw-a wa-na-vyo-LIM-a Ukiangalia kwa makini, utaona kuna sehemu ya kitenzi hiki ambayo haibadiliki katika mifano ya hapo juu. Sehemu hiyo ni (-LIM-). Na hii ndiyo shina au mzizi wa kitenzi LIMA. Mfano mwingine: a-li-ki-SOM-a hu-SOM-ew-a wa-li-SOM-e-an-a a-li-m-SOM-e-a i-li-SOM-w-a Tunaona hapa mzizi/shina la kitenzi SOMA, ni -som- Ili utambue shina/mzizi wa kitenzi unafaa kuwazia hali mbalimbali au kauli tofautitofauti za mnyambuliko wa kitenzi halafu ubainishe sehemu isiyobadilika.