Kiditammari
Kiditammari ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Benin na Togo inayozungumzwa na Waditammari. Mwaka wa 2006 idadi ya wasemaji wa Kiditammari nchini Benin imehesabiwa kuwa watu 120,000. Pia kuna wasemaji 27,500 nchini Togo. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiditammari kiko katika kundi la Kigur.
Viungo vya nje [hariri]
- lugha ya Kiditammari kwenye Multitree
- ramani ya Kiditammari
- http://www.ethnologue.org/show_language.asp?code=tbz
Viambishi ni mofimu au viungo vyenye maana ambavyo hufungamanishwa na mzizi/shina la neno ili kulipa neno hilo maana mbalimbali za kisarufi kama vile nafsi, wakati, hali, urejeshi, n.k Viambishi awali ni vile vinavyotangulia mzizi wenyewe, yaani huwa kabla ya mzizi/shina. SHINA AU MZIZI: Hakuna tofauti kati ya shina na mzizi MZIZI/SHINA, Ni sehemu ya neno inayobeba maana yake kuu na huwa haibadiliki, Kwa mfano, tuangalie vitenzi vifuatavyo: a-na-LIM-a wa-li-LIM-i-a ni-ta-LIM-iw-a wa-na-vyo-LIM-a Ukiangalia kwa makini, utaona kuna sehemu ya kitenzi hiki ambayo haibadiliki katika mifano ya hapo juu. Sehemu hiyo ni (-LIM-). Na hii ndiyo shina au mzizi wa kitenzi LIMA. Mfano mwingine: a-li-ki-SOM-a hu-SOM-ew-a wa-li-SOM-e-an-a a-li-m-SOM-e-a i-li-SOM-w-a Tunaona hapa mzizi/shina la kitenzi SOMA, ni -som- Ili utambue shina/mzizi wa kitenzi unafaa kuwazia hali mbalimbali au kauli tofautitofauti za mnyambuliko wa kitenzi halafu ubainishe sehemu isiyobadilika.