Kibissa
Kibissa ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Burkina Faso, Ghana na Cote d'Ivoire inayozungumzwa na Wabissa. Mwaka wa 1999 idadi ya wasemaji wa Kibissa nchini Burkina Faso imehesabiwa kuwa watu 350,000. Pia kuna wasemaji 166,000 nchini Ghana (2003), 63,000 nchini Cite d'Ivoire (Wabissa wahamiaji tu) na 3000 nchini Togo. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibissa kiko katika kundi la Kimande.
Viungo vya nje[hariri]
- lugha ya Kibissa kwenye Multitree
- ramani ya Kibissa
- http://www.ethnologue.org/show_language.asp?code=bib
Viambishi ni mofimu au viungo vyenye maana ambavyo hufungamanishwa na mzizi/shina la neno ili kulipa neno hilo maana mbalimbali za kisarufi kama vile nafsi, wakati, hali, urejeshi, n.k Viambishi awali ni vile vinavyotangulia mzizi wenyewe, yaani huwa kabla ya mzizi/shina. SHINA AU MZIZI: Hakuna tofauti kati ya shina na mzizi MZIZI/SHINA, Ni sehemu ya neno inayobeba maana yake kuu na huwa haibadiliki, Kwa mfano, tuangalie vitenzi vifuatavyo: a-na-LIM-a wa-li-LIM-i-a ni-ta-LIM-iw-a wa-na-vyo-LIM-a Ukiangalia kwa makini, utaona kuna sehemu ya kitenzi hiki ambayo haibadiliki katika mifano ya hapo juu. Sehemu hiyo ni (-LIM-). Na hii ndiyo shina au mzizi wa kitenzi LIMA. Mfano mwingine: a-li-ki-SOM-a hu-SOM-ew-a wa-li-SOM-e-an-a a-li-m-SOM-e-a i-li-SOM-w-a Tunaona hapa mzizi/shina la kitenzi SOMA, ni -som- Ili utambue shina/mzizi wa kitenzi unafaa kuwazia hali mbalimbali au kauli tofautitofauti za mnyambuliko wa kitenzi halafu ubainishe sehemu isiyobadilika.