Kibeti (Cote d'Ivoire)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kibeti (pia Kieotile) ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Cote d'Ivoire inayozungumzwa na Wabeti. Isichanganywe na lugha ya Kibeti nchini Kamerun. Mwaka wa 1999 idadi ya wasemaji wa Kibeti imehesabiwa kuwa watu 200 tu. Wabeti wengi wameanza na kuzidi kutumia lugha ya Kianyin badala ya Kibeti. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibeti iko katika kundi la Kikwa.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kibeti (Cote d'Ivoire) kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.