Kassim Bizimana
| Kassim Bizimana | ||
| Maelezo binafsi | ||
|---|---|---|
| Jina kamili | Kassim Bizimana | |
| Tarehe ya kuzaliwa | 29 Desemba 1985 | |
| Mahala pa kuzaliwa | Bujumbura, Burundi | |
| Nafasi anayochezea | Mshambuliaji | |
| Maelezo ya klabu | ||
| Klabu ya sasa | BV Veendam | |
| Namba | 19 | |
| Klabu za ukubwani | ||
| Miaka | Klabu | |
| 2005 | BV Veendam | |
| Timu ya taifa | ||
| 2008 | Burundi | |
|
* Magoli alioshinda |
||
Kassim Bizimana (amezaliwa 29 Desemba 1985 katika mji wa Bujumbura) ni mchezaji wa mpira, hasa mshambuliaji kutoka nchi ya Burundi. Anaichezea klabu ya BV Veendam katika ligi ya pili Uholanzi (kwa Kiholanzi Eerste Divisie). Aliichezea nchi yake ya Burundi katika mechi za kimataifa. Mwaka wa 2007 timu ya kitaifa ya Rwanda ilijaribu kumuomba achezee timu ya Taifa ya Rwanda lakini mchezaji huyo alichagua kuichezea timu ya Burundi.
Kassim Bizimana ana paspoti ya kiholanzi na hiyo ni kutokana na muda mrefu ameishi huko Uholanzi.
Kucheza kwake Ulaya [hariri]
Bizimana alichezea klabu za vijana za SC Heerenveen na Achilles 1894. Alianza kuwa mchezaji wa kulipwa mwaka 2004 kwenye klabu ya FC Groningen. Mechi yake ya kwanza kabisa na klabu yake hiyo ilikuwa tarehe 22 Oktoba 2004 dhidi ya Willem II Tilburg pindi alipomgomboa mchezaji (Jack Tuyp) katika dakika ya 74. Groningen ilifungwa 4-2.
Katika Julai 2005, aliuzishwa katika klabu ya BV Veendan. Bizimana alionekana kuwa mchezaji mzuri na anashiriki dakika nyingi na timu yake hiyo na ni kiungo muhimu sana katika klabu yake hiyo na kwa sasa ndio timu anayoichezea.
Bizimana ana mechi 13 katika timu yake ya taifa ya Burundi na ana magoli manne.
Viungo vya nje [hariri]
- www.bvveendam.nlKassim katika tovuti ya klabu yake
- ProfileMchezaji katika National football teams
- Voetbalnext ProfileKatika Voetbalnext Kiholanzi
- Cartera de Futbolistas Profile
- Voetbal International Profile
- Statistics