Kasimir Mtakatifu
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mtakatifu Kasimir (kwa Kipolandi Kazimierz) alikuwa muungwana kutoka nchi ya Poland, alipozaliwa mjini Krakow tarehe 3 Oktoba, 1458, akafariki mjini Grodno (leo nchini Belarus) tarehe 4 Machi, 1484). Tarehe ya kifo chake, yaani 4 Machi pia ni sikukuu yake.
Ametambuliwa na Kanisa Katoliki chini Papa Adrian VI kuwa mtakatifu kuanzia mwaka wa 1522.
[hariri] Maisha
Kasimir alizaliwa mwaka 1458. Baba yake alikuwa mfalme wa Poland.
Katika maisha yake alidhihirisha fadhila za Kikristo, hasa usafi wa moyo na upendo kwa maskini. Alikuwa na imani thabiti, na aliheshimu sana Ekaristi na Mama Bikira Maria. Alikufa mapema kwa ugonjwa mwaka 1484.
[hariri] Tazama pia
[hariri] Marejeo
- "Sala ya Kanisa - Vipindi vya Liturjia", Toleo la Tatu 1996, Ndanda - Peramiho: Benedictine Publications, uk.1296
| Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kasimir Mtakatifu kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |