Kasanga (Ufipa)
| Kasanga | |
| Nchi | Tanzania |
|---|---|
| Mkoa | Rukwa |
| Wilaya | Sumbawanga Vijijini |
Kasanga ni mji mdogo upande wa Kusini-Magharibi wa Tanzania mwambaoni kwa Ziwa Tanganyika. Ni kata ya wilaya ya Sumbawanga Vijijini yenye wakazi 25,831.
Wakati wa koloni ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani Kasanga iliitwa "Bismarcksburg" (kwa heshima ya chansela Mjerumani Otto von Bismarck). 1913 Bismarckburg ilipandishwa cheo kuwa makao makuu ya mkoa wa 12 wa koloni ikawa mji mkuu wa mkoa mkubwa wa pili katika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani iliyojumlisha maeneo ya Ufipa, Ukonongo, Ugala na Uwende.
Baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia jina la Kijerumani lilibadilishwa na Waingereza kuwa Kasanga.
Kuna mipango ya kuboresha bandari ya Kasanga na kuiunganisha na barabara ya lami.
| Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Rukwa bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kasanga (Ufipa) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
| Kata za Wilaya ya Sumbawanga Vijijini – Mkoa wa Rukwa - Tanzania | ||
|---|---|---|
|
Kaengesa | Kalambazite | Kaoze | Kasanga (Ufipa) | Katazi | Kipeta | Laela | Legezamwendo | Lusaka (Rukwa) | Mambwekenya | Mambwenkoswe | Matai | Miangalua | Milepa | Mkowe | Mpui | Msanzi | Mtowisa | Muze | Mwazye | Mwimbi | Sandulula | Sopa |
||