Karoli Borromeo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Karoli Borromeo

Karoli Borromeo (2 Oktoba, 15383 Novemba, 1584) alikuwa kardinali na askofu wa Milano nchini Italia. Ametambuliwa na Kanisa Katoliki kuwa mtakatifu. Sikukuu yake ni 4 Novemba.

[hariri] Maisha

Karoli Borromeo alizaliwa katika mji wa Arona katika mkoa wa Lombardia nchini Italia mwaka 1538.

Baada ya kupata shahada ya tatu katika sheria za serikali na za Kanisa, alifanywa kardinali na mjomba wake, Papa Pius IV, akachaguliwa kuwa askofu wa Milano.

Alikuwa mchungaji bora wa kundi lake. Mara kwa mara alipita kote jimboni mwake, aliitisha mikutano, aliweka sheria za kufaa kwa watu, na alijitahidi kuhimiza maadili ya Kikristo.

Ndiye aliyefanikisha zaidi sehemu ya mwisho wa Mtaguso wa Trento na utekelezaji wake, kama vile uanzishaji wa seminari kwa ajili ya malezi ya mapadri wapya.

Alianzisha pia shirika la Oratorio.

Alikufa tarehe 3 Novemba 1584.

[hariri] Tazama pia

[hariri] Marejeo

  • "Sala ya Kanisa - Vipindi vya Liturjia", Toleo la Tatu 1996, Ndanda - Peramiho: Benedictine Publications, uk.1562


Christian cross.svg Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Karoli Borromeo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.