Kanisa la Kitume la Armenia
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kanisa la Kitume la Armenia (kwa Kiarmenia: Հայ Առաքելական Եկեղեցի), ambalo pengine linaitwa pia Kanisa la Kiorthodoksi la ArmenIa au Kanisa la Kigregori, ni Kanisa la kitaifa la kale zaidi duniani (301).
Wafuasi wake wanahesabiwa kati ya Waorthodoksi wa Mashariki kwa sababu hawakubali mtaguso wa Kalsedonia na ile iliyofuata.
Mkuu wake anaitwa Catholikos (kwa Waarmenia cheo hicho ni cha juu kuliko kile cha "Patriarki") na makao yake makuu yako Echmiadzin, huko Armenia. Kwa sasa ni Karekin II.
Yupo pia Catholikos mwingine mwenye makaO makuu Antilyas huko Lebanoni. Kwa sasa ni Aram I.