Kanisa Katoliki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kanisa la Kikatoliki)
Rukia: urambazaji, tafuta
Papa Fransisko akiendesha Misa ya kuanzia rasmi huduma yake kama askofu wa Roma na mkuu wa Kanisa Katoliki duniani kote, tarehe 19 Machi 2013.
Hii ni sehemu ya mfululizo kuhusu
Kanisa Katoliki
StPetersBasilicaEarlyMorning.jpg
Imani

Umoja wa Mungu
Utatu (Baba, Mwana, Roho Mtakatifu)
Umwilisho Maisha ya Yesu
Msalaba Ufufuko Kupaa
Historia ya Wokovu Ufunuo
Biblia Mapokeo Ualimu Dogma
Neema Dhambi Wokovu Sakramenti
Watakatifu Bikira Maria


Muundo

Papa: Benedikto XVI
Urika wa maaskofu Mitaguso mikuu
Kundi la Makardinali
Kanisa la Kilatini
Makanisa Katoliki ya Mashariki

Historia

Historia Ukristo
Ukatoliki Mlolongo wa Kitume
Sifa nne za Kanisa Utetezi Ekumeni
Maisha ya kiroho Amri Kumi Utawa
Sala Falsafa Teolojia
Muziki Sanaa Sayansi

Ibada

Liturujia Mwaka wa Kanisa
Ekaristi Liturujia ya Vipindi

Mapokeo ya liturujia

Liturujia ya Kilatini (Roma Milano Toledo Braga Lyon Canterbury)
Liturujia ya Armenia Liturujia ya Misri
Liturujia ya Ugiriki Liturujia ya Antiokia
Liturujia ya Mesopotamia

Kanisa Katoliki ni jina linalotumika hasa kumaanisha Kanisa la Kikristo linalokubali mamlaka ya kiroho ya Papa wa Roma kama mkuu wa urika wa Maaskofu juu yake lote. Ndilo kubwa kabisa kati ya madhehebu yote ya dini hiyo, likikusanya nusu ya wafuasi wote wa Yesu.

Yaliyomo

Maana ja jina [hariri]

Neno "katoliki" linatokana na kivumishi cha Kigiriki καθολικός (katholikòs), lenye maana ya «kamili, kadiri ya utimilifu». Tunalikuta kwa mara ya kwanza katika maandishi ya Ignas wa Antiokia kwa Wakristo wa Smirna mwanzoni mwa karne II: «Alipo Yesu Kristo ndipo lilipo Kanisa Katoliki» (Ad Smyrnaeos, 8).

Imani yake [hariri]

Kanisa hilo linaamini kuwa ndani yake linadumu moja kwa moja Kanisa pekee lililoanzishwa na Yesu Kristo ambalo wanaunganishwa nalo wote wanaobatizwa katika madhehebu yoyote.

Tofauti ni kwamba baadhi (Wakatoliki) wana ushirika kamili nalo, wakati wengine (hasa Waorthodoksi na Waprotestanti) wana ushirika nalo kwa viwango mbalimbali, kadiri wanavyokubali mafundisho, sakramenti na uongozi wake.

Uenezi wake [hariri]

Kati ya madhehebu ya Kikristo, Kanisa Katoliki linakusanya waamini 1,214,000,000, yaani nusu ya wafuasi wote wa Yesu, na 17.5 % ya binadamu wote, likiwa na asilimia kubwa ya waamini kati ya wananchi wa Amerika na Ulaya.

Miundo yake [hariri]

Kanisa Katoliki linaishi katika majimbo 2,979, ambayo kwa kawaida yanaongozwa na Maaskofu (kwa jumla wako 5,132) wakisaidiwa na mapadri (413,418) na mashemasi, ambao baadhi yao wanajiandaa kupata upadrisho na 41,000 hivi ni wa kudumu.

Kati ya majimbo hayo, mengi yanafuata utaratibu wa Kanisa la Kilatini, ila kuna mengine yanayofuata taratibu za Makanisa Katoliki ya Mashariki.

Majimbo yanagawanyika katika parokia zinazoongozwa na padri anayeitwa paroko.

Kati ya waamini, ambao wengi kabisa kati yao ni wale wa kawaida wanaoitwa walei, wana nafasi ya pekee wamonaki na watawa wengine ambao wanaishi kwa mitindo mbalimbali iliyostawi katika historia ya Kanisa ili kumfuata Yesu kwa karibu zaidi katika useja mtakatifu, ufukara na utiifu, kadiri ya karama maalumu. Masista ni 713,000 hivi na mabruda 55,000.

Asilimia ya Wakatoliki waliobatizwa kati ya wakazi wa kila nchi.
Icon-religion.png Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kanisa Katoliki kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.