Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
| Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania | |
|---|---|
| Mkuu wa kanisa: | Alex Gehaz Malasusa |
| Uhusiano: | All Africa Conference of Churches (AACC) Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) World Lutheran Federation |
| Idadi ya dayosisi: | 20 |
| Wanachama: | Milioni 4,6 |
| Anuani ya barua: | P.O. Box 3033 Arusha, Tanzania |
| Tovuti rasmi: | http://www.elct.org/ |
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ni muungano wa Kilutheri katika nchi ya Tanzania. Mwaka 1938 makanisa saba ya Kilutheri yaliungana kama Muungano wa Makanisa ya Kilutheri, na tarehe 19 Juni 1963 yalikuwa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania.[1]
Lengo la KKKT ni kuwapa watu nafasi ya kumfahamu Yesu Kristo ili kupata maisha ya milele. Kanisa limejengwa juu ya msingi wa Yesu Kristo, limeongozwa na Neno la Mungu (Biblia) kama linapatikana katika Agano la Kale na Agano Jipya, na limeimarishwa katika sakramenti.
KKKT linaongozwa na Mkuu wa kanisa (askofu Mkuu) na maaskofu ishirini kutoka dayosisi ishirini, wakiwa na wanachama zaidi ya milioni 4,6.
Ofisi kuu wa KKKT imo katika mji wa Arusha. KKKT linalo uhusiano na All Africa Conference of Churches (AACC), Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Lutheran World Federation (LWF) na Lutheran Mission Cooperation (LMC).
KKKT ni chama kinachowapa wanachama chake nafasi ya kumwabudu Mungu, kupata elimu ya Kikristo na huduma nyingi nyingine.
Yaliyomo |
[hariri] Matawi
- Elimu (Sekondari and Chuo Kikuu)
- Fedha na Utawala
- Afya na Utibabu (Mahospitali 21 na zahanati nyingi)
- Umisheni na Uinjilisti
- Upangaji na Maendeleo
- Hudumu ya Jamii na Kazi ya Akinamama
[hariri] Dayosisi
|
[hariri] Viuongo vya nje
- (Kiingereza) Evangelical Lutheran Church in Tanzania Tovuti rasmi ya KKKT
- (Kiingereza) Lutheran Mission Cooperation Tovuti rasmi ya LMC
[hariri] Notes
- ↑ Homepage. Evangelical Lutheran Church in Tanzania (2007). Retrieved on 2008-12-17.
- ↑ http://www.elct-ned.org/
- ↑ http://www.elct-nwd.org/
