Kanghagha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Kanghagha
Kanghagha uso-mweusi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Sylvioidea (Ndege kama kucha)
Familia: Timaliidae (Ndege walio na mnasaba na kanghagha)
Jenasi: Alcippe Blyth, 1844

Babax David, 1875
Cutia Hodgson, 1837
Dryonastes Sharpe
Garrulax Lesson, 1831
Grammatoptila Reichenbach, 1850
Ianthocincla Gould, 1835
Kupeornis Serle, 1949
Leucodioptron Blyth, 1860
Melanocichla Sharpe, 1883
Phyllanthus Lesson, 1844
Pterorhinus Swinhoe, 1868
Ptyrticus Hartlaub, 1883
Rhinocichla Sharpe, 1883
Stactocichla Sharpe, 1883
Strophocincla
Trochalopteron Blyth, 1843
Turdoides Cretzschmar, 1827

Kanghagha au zogoyogo ni ndege wa familia Timaliidae. Wanafanana na mikesha wa familia Turdidae. Wanatokea misitu na maeneo mengine yenye miti katika Afrika na Asia. Spishi za Afrika zina rangi za kahawa, nyeusi, kijivu na nyeupe, lakini spishi nyingi za Asia zina rangi kali pia kama nyekundu na njano. Takriban spishi zote huenda kwa makundi wakiwasiliana kwa sauti. Mara kwa mara hupiga kelele sana, kwa sababu yake huitwa mpayupayu pia (“babbler” au “chatterer” kwa Kiingereza). Hula wadudu hasa lakini beri pia; spishi kubwa hula mijusi na panya wadogo na spishi kadhaa hula beri tu. Hulijenga tago lao kwa vitawi na kulificha katika vichaka vizitu. Jike huyataga mayai 2-5. Spishi kadhaa hujenga tago kwa kundi; jike mmoja tu hutaga mayai na ndege wengine husaidia kuwalinda makinda na kuwaletea chakula.

[hariri] Spishi za Afrika

[hariri] Spishi za Asia

[hariri] Picha

Vifaa binafsi
Maeneo ya wiki

Vibadala
Vitendo
Urambazaji
Vifaa
Lugha zingine