Kampuni ya Kittinger

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kampuni ya Kittinger
Jina la kampuni Kampuni ya Kittinger
Ilianzishwa Buffalo, New York, 1866
Huduma zinazowasilishwa Uuzaji na utengenezaji
Mmiliki Raymond Bialkowski, Rais na Mkurugenzi mkuu
Aina ya kampuni Biashara ya familia
Makao Makuu ya kampuni Buffalo,NY, Marekani
Bidhaa zinazosambazwa na kampuni hii Fanicha za nyumba na za kuagizwa kibinafsi
Nchi MarekaniMarekani
Tovuti http://www.kittingerfurniture.com

Kampuni ya Kittinger ni kampuni ya Marekani ya kuunda samani za kikoloni.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Kampuni ilianzishwa katika mwaka wa 1866 Buffalo, New York. Kutoka mwaka wa 1937 hadi 1990, ilikuwa kampuni kuu ya kuunda fanicha ya Shirika la Colonial Williamsburg Foundation na pia ,iliuza samani ya muundo wa Williamsburg kwa wageni kutoka nyumba ya Williamsburg Reproductions,nyumba iliitwa Craft House.Hasa kumaanisha nyumba ya sanaa. Kama kampuni ya fanicha ya Biggs Furniture ya Richmond,Virginia,Kittinger ilihudumia wananchi walio katika daraja la katikati kiuchumi.Waliuunda samani wakitumia mbao ngumu ile iwe na ubora sawa kama samani ya awali ya ukoloni. Bidhaa zao ziliundwa katika mitindo ya Queen Anne, Chippendale na Hepplewhite.

Idadi kubwa ya samani za Kittinger inapatikana katika sehemu ya West Wing katika jumba la White House huko Washington,DC.Wafanyikazi wa kupamba ndani ya nyumba wa Colonial Williamsburg Foundation walipewa kazi na Rais Richard Nixon ya kupamba ofisi za Rais. Kampuni ya Kittinger ndiyo iliyofanya kazi hii kwa sababu hii ndiyo kampuni pekee iliyoundia Colonial Williamsburg Foundation samani zao zinazofanana na zile za karne ya kumi na nane.. Katika muundo mpya wa ofisi zile,kuliongezwa meza ya mkutano na viti vya chumba cha mawaziri. Rais Nixon alilipa kwa hundi ya kibinafsi kulipia meza ile iliyoundwa na kampuni ya Kittinger na wakapatia White House. Kampuni inaendelea katika kazi ya utengenezaji huko Buffalo, NY.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. ^ Pollard, Garland (2004-03-01). "Colonial Williamsburg, its history". Archived 17 Oktoba 2007 at the Wayback Machine. brandchannel.com. Interbrand.
  2. ^ "Archives: Case Pieces". Americana Furniture and Interiors.
  3. ^ "Douglas W. Kenyon Biography". Archived 16 Novemba 2007 at the Wayback Machine. Hunton and Williams.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]