Kampuni ya Bacup
| Kampuni ya Viatu ya Bacup | |
|---|---|
| Jina la kampuni | Kampuni ya Viatu ya Bacup |
| Ilianzishwa | 1928 |
| Mwanzilishi | Ernst Goodwin |
| Huduma zinazowasilishwa | Utengenezaji |
| Makao Makuu ya kampuni | Lancashire,Uingereza |
| Bidhaa zinazosambazwa na kampuni hii | Viatu |
| Nchi | Uingeeza |
| Tovuti | Tovuti rasmi ya Kampuni ya Bacup |
Yaliyomo |
Muhtasari [hariri]
Kampuni ya Viatu ya Bacup ni kampuni ya kutengeneza viatu iliyo na makao yake katika kijiji cha Stacksteads,karibu na Bacup, Lancashire,Uingereza. Kampuni hii ilianzishwa katika mwaka wa 1928 na Ernst Goodwin. Kampuni ya Bacup ni mojawapo ya kampuni bora, zinazojulikana kwa kuunda viatu, zilizofunga viwanda vyake katika mwisho wa miaka ya 1990 na kuanza kuagiza viatu kutoka Mashariki ya Mbali. Wanaowasilisha viatu hivyo wana makao yao nchini Uchina(nchi ambayo kampuni hii imeanzisha makao yake mpya),Vietnam na Uhispania.[1]
Ukuaji wa Kampuni ya Viatu ya Bacup [hariri]
Tangu mwaka wa 1928, kampuni hii imenawiri na ikawa wasambazaji wengi, wa viatu vyao, katika nchi ya Uingereza.Makao yao makuu yalipatikana Stacksteads.
Sekta kuu za kampuni hii ni viatu vya Wanaume, Wanawake, Watoto na vya kutumika katika mazoezi ya michezo. Wameajiri wauzaji wa rejareja wanaojulikana sana kwa mfano Tesco,ASDA ,Woolworths na Littlewoods wakiwa wateja wao wakuu.
Katika mwaka wa 2002,kampuni hii ilifungua sehemu mpya iliyoitwa Alpha Logistics & Warehousing ya kuhusisha matumizi kamili ya maghala yao yote na matumizi bora ya wafanyikazi wenye vipaji.
Pamoja na upanuzi wa makao makuu ya kampuni hii,Bacup wameanzisha aina mpya ya viatu vya wasichana.Aina hii inaitwa Redfoot After Party Shoe na ni bidhaa za kampuni hii zilizosajiliwa katika sheria.
Marejeo [hariri]
- ^ Wide Fitting Famous Footwear and Famous Foot Care Products by - Natureform.co.uk
- ^ Lancashire County Council: Lancashire Profile
- ^ Retailing - UK News 1998
- ^ SHOEINFONET Wanted - Employee
- ^ Bacup Shoes