Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Tuzo Nobel.png

Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) ni shirika la kimataifa ambalo ofisi yake kuu iko Geneva, Uswisi.

Kamati ilianzishwa na Henri Dunant kwa jina Kamati ya Watano tarehe 9 Februari 1863.

Shabaha zake hasa ni kuwasaidia na kuwalinda watu wakati wa vita.

Kamati imezawadiwa Tuzo ya Nobel ya Amani mara tatu: miaka ya 1917, 1944, na 1963.

Siku hizi, kamati ni mwanachama wa Shirika za msalaba mwekundu na hilali nyekundu.