Kalebezo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kalebezo ni kata ya Wilaya ya Buchosa katika Mkoa wa Mwanza, Tanzania. Msimbo wa posta ni 33308.

Kata ya Kalebezo inaundwa na vijiji vitano ambavyo ni: Nyashana, Katoma, Magulukenda, Busekeseke na Kalebezo. Makao makuu ya kata yapo kijiji cha Kalebezo. Ni wastani wa Km 10 kufika ziwa Viktoria.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 19,684 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 18,960 waishio humo.[2]

Asili ya jina "Kalebezo" ni kilima kilicho misheni ya Wakatoliki eneo hilo la kilima. Watu walilitumia kama dira kuonea maeneo mbalimbali ya vijiji jirani hata mtu kuelekezwa uelekeo. Jina linatokana na lugha ya Kizinza ikiwa na maana ya "Pakuonea".

Kijiji cha Kalebezo kilibahatika kupata wamisionari wa White Fathers: hao walijenga parokia kijijini hapo na baadaye watawa wa Maryknoll Sisters mwaka 1998 wakajenga kituo cha Vema ambacho kilikuwa ni chuo cha ufundi; hata hivyo baadaye kilifungwa.

Kata ya Kalebezo hupata mvua za kutosha: ni maarufu kwa mazao ya mpunga, mahindi, mihogo na mtama. Aidha kuna ufugaji kiasi.

Kata ya Kalebezo ina jumla ya shule za msingi 7 na shule shikizi 1. Shule za Sekondari zilizopo ni mbili: Kalebezo Sekondari iliyoanza mwaka 2005 na Magulukenda Sekondari iliyoanza mwaka 2012 chini ya diwani Joseph Yaredi.

Upande wa huduma za afya kata ya Kalebezo kuna zahanati 3: Busekeseke, Katoma na Kalebezo.

Kata ya Kalebezo imepata nishati ya umeme na kwa kijiji cha Kalebezo kuna maji ya bomba kutoka Ziwa Viktoria.

Mitandao ya simu inakamata wastani: baadhi ya maeneo kuna changamoto ya mawasiliano. Minara mingi ipo makao makuu ya Halmashauri ya Buchosa, Nyehunge.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Kata za Wilaya ya Buchosa - Mkoa wa Mwanza - Tanzania

Bangwe | Bugoro | Buhama | Bukokwa | Bulyaheke | Bupandwa | Iligamba | Irenza | Kafunzo | Kalebezo | Kasisa | Katwe | Kazunzu | Lugata | Luharanyonga | Maisome | Nyakaliro | Nyakasasa | Nyakasungwa | Nyanzenda | Nyehunge

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mwanza bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kalebezo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.