Kalasinga
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kalasinga (Kipunjabi ਸਿੱਖੀ sikhi; pia: Usikhi) ni dini yenye asili ya Uhindi inayomwabudu Mungu mmoja.
Wafuasi wake huitwa Kalasinga au Sikh na kitabu kitakifu chao ni Guru Granth Sahib. Idadi ya wafuasi ni takriban milioni 20 na wengi wao wanaishi Uhindini katika jimbo la Punjab. Kutokana na uhamiaji kuna pia jumuiya za Kalasinga huko Uingereza, Afrika ya Mashariki, Kanada na sehemu mbalimbali za dunia.
Kalasinga ilianzishwa katika karne ya 15 na Guru Nanak aliyezaliwa katika familia ya Kihindu wakati wa utawala wa Waislamu juu ya Uhindi ya kaskazini. Nanak alijishughulihsa na dini tangu utoto na kwenye umri wa miaka 30 aliondoka katika familia alianza kipindi kirefu cha matembezi. Anasemekana alizunguka kote Uhindi akafika pia Makka, Uajemi na Afghanistan. Hakukubali ibada nyingi za Uhindu, mafundisho na maandiko ya kidini, tabaka za kijamii. Alisikitika kuona jinsi gani dini ilivyogawa watu.
Hapa alianza kufundisha dini ya umoja. Wataalamu wengine wameeleza mafundisho yake kama jaribio la kuondoa matatatizo kati ya Waislamu na Wahindu kwa kutafuta imani ya pamoja iliyojengwa kwenye misingi ya Uhindu lakini kupokea mengi kutoka Uislamu.
Guru Nanak alifuatwa na maguru tisa wengine. Katikia kipindi hiki polepole Kalasinga waliendelea kuwa jumuiya ya pekee. Waliteswa na na watawala wa Kihindu lakini zaidi na watawala Waislamu. Walianza kubeba silaha na kujitetea na kuwa kundi muhimu katika Punjab.
[hariri] Kaakar tano
Tangu guru ya kumi Gobind Singh walionekana kabisa kama kundi la kidini la pekee. Wanaume hufuata kanuni za "Kaakar tano":
- kes: nywele ndefu; hawakati nywele wala ndevu wakionyesha ya kwamba kila kitu kilichoumbwa na Mungu ni kizuri
- kangha: chanuo dogo - nyele zinatakiwa kutunzwa vizuri
- kara: bangili ya chuma - alama ya kuwa mali ya guru
- kirpan: upanga mdogo - wawe tayari kutetea imani na haki
- kaccha: chupi - inamkumbusha sikhi ya kwamba anahitaji kutawala tamaa zake za kimwili
Sharti ya kuktokata nywele imesababisha alama ya nje ya Kalasinga yaani kilembe kwa sababu nywele za kichwa pamoja na ndevu hufungwa katika kilembe na Kalasinga huonekana kirahisi kutokana vilembe vyao.
[hariri] Imani kadhaa
Kati ya mafundisho ya kimsingi ni imani katika Mungu mmoja anayeitwa Waheguru. Kama Wahindu wanaamini ya kwamba nafsi ya mtu huzaliwa upya tean na tena na shabaha ya dini ni ukombozi katika mzunguko wa kuzaliwa upya na upya tena. Ukobozi wanaona katika jina la Mungu na jitihada za kujisafisha kiroho. Waheguru au Mungu hana umbo na hawezi kuelezwa na akili ya kibinadamu.
- Mungu mmoja tu. Aliumba ulimwengu, anaitunza na mwenye uwezo wa kuumaliza.
- Mungu haingii katika maumbile ya kibinadamu.
- Shabaha ya maisha ni kujiondoa katika giza ya kiroho na mapendzi ya vitu vya kidunia. Njia yake ni kutakarai na kutamka jina la Mungu.
- Guru wa pekee ni kitabu kitakatifu cha Guru Granth Sahib
- Wanawake ni sawa na wanaume
- Kila kalasinga anatkiwa kuchapa kazi na kuwa mwaninifu
- Wote wanatakiwa kushirikiana mafanikio ya kazi yao
- kila mmoja anatakiwa kumsaidia mwenzake na hasa mwenye matatizo
[hariri] Viungo vya Nje
- Sikhs.org
- Sikh Missionary Society (UK) — Non-profit organization dedicated to promoting the Sikh religion, culture and history
- Religious Tolerance
- BBC
- Siknet
- Sikh Wiki

