Kaizari Joseph II

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Joseph II alivyochorwa na Anton von Maron, 1775.

Joseph II (13 Machi 174120 Februari 1790) alikuwa Kaizari wa Dola la Ujerumani kuanzia 1765 hadi kifo chake. Alimfuata baba yake, Francis I, na kufuatwa na mdogo wake, Leopold II.

Sera zake katika utawala Austria peke yake miaka 1780-1790 zimeitwa Ujosefu (au Josefini). Sera hizo zilifuata falsafa ya mwangaza na kuingilia na kubana mamlaka ya Kanisa katika mambo mengi, hata madogo sana.

Kwa sababu hiyo alilaumiwa vikali na Kanisa Katoliki na kuhusianishwa na tapo la Wamasoni.

Pamoja na hilo, alipatwa na upinzani mkubwa, na hatimaye alifuta baadhi ya maamuzi yake.

Alipokufa, Leopoldo II alizidi kurudisha mambo yalivyokuwa awali na kujali hisia za wananchi.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Berenger, Jean (1990), A History of the Habsburg Empire, 1700-1918, Edinburgh: Addison Wesley 
  • Ingrao, Charles W. (2000), The Habsburg Monarchy, 1618-1815, New York: Cambridge University Press 
  • Kann, Robert (1974), A History of the Habsburg Empire, 1526-1918, Los Angeles: University of California P 
  • Okey, Robin (2002), The Habsburg Monarchy c. 1765-1918, New York: Palgrave MacMillan 
Makala hii kuhusu Kaizari fulani wa Ujerumani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kaizari Joseph II kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.