Kaduna

Majiranukta: 10°31′N 7°26′E / 10.517°N 7.433°E / 10.517; 7.433
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Kaduna
Majiranukta: 10°31′23″N 7°26′25″E / 10.52306°N 7.44028°E / 10.52306; 7.44028
Country Nigeria
State Kaduna
Serikali
 - Governor Mohammed Namadi Sambo
Eneo
 - Jumla (3,080 km²)
Idadi ya wakazi (2006)
 - Wakazi kwa ujumla 1,458,900
 - Ethnicities Hausa
CET (UTC+1)
 - Summer (DST) CEST (UTC+1)
Tovuti:  http://www.kadunastate.gov.ng/
Mto Kaduna.

Kaduna ni mji mkuu wa jimbo la Kaduna kaskazini-kati mwa Nigeria. Mji huo, ambao uko kwenye Mto wa Kaduna, ni kiini cha biashara kubwa na usafiri kwa maeneo ya kilimo yaliyo karibu pamoja na reli na makutano ya barabara.

Idadi ya wakazi wa Kaduna ni 8,252,400.

Ishara ya Kaduna ni mamba, aitwaye Kada katika lugha ya Kihausa .

Historia[hariri | hariri chanzo]

Kaduna ilianzishwa na Waingereza mwaka wa 1913 na kuwa mji mkuu wa Nigeria wa zamani wa Mkoa wa Kaskazini mwaka 1917. [1] Ilihifadhi hali hiyo mpaka 1967.

Watu waliotoka Kaduna ni pamoja na Emmanuel na Celestine Babayaro (wachezaji mpira wa Nigeria) na Fiona Atlanta (mwanasinema wa Uingereza na msichana katika sinema ya Bond)

Ugomvi wa Kidini[hariri | hariri chanzo]

Kaduna imekuwa mahala pa mvutano wa kidini kati ya Waislamu na Wakristo, hasa juu ya utekelezaji wa sheria katika shari'a katika mji wa Kaduna mwanzo wa mwaka wa 2001. Hasa katika tukio moja Februari mwaka wa 2000 angalau watu 1,000 waliuawa katika zogo fulani. Mji unabakia umetengwa siku hizi, ambapo Waislamu hasa wanaishi kaskazini mwa mji na Wakristo kusini. [2] Tukio jingine lilitokana na makala katika gazeti Lagos ambayo yalitia Waislamu hasira. Makala ilikuwa juu ya shindano la kutafuta Mrembo wa Dunia lililokuwa wiki hiyo katika mji mkuu wa Abuja, kupendekeza kwamba kama Muhammad angehudhuria shindano hilo angeweza kuoa mmoja wa washindani hao. [3]

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Kaduna ni nyumbani mwa Chuo cha Ulinzi cha Nigeria (1964), Kaduna Polytechnic (1968), Chui kikuu cha Ahmadu Bello (1962), Chuo kikuu cha Kaduna(2007), Chuo cha Urobani na Teknolojia cha Nigeria na Taasisi ya Utafiti wa Trypanosomiasis Nigeria (1951).

Uchumi na usafiri[hariri | hariri chanzo]

Kaduna ni kituo cha viwanda Kaskazini mwa Nigeria, vinatengeneza bidhaa kama nguo, mashine, chuma, alumini, bidhaa za mafuta na magurudumu.

Ufinyaji wa Udongolinalofanywa sana katika Kaduna, hasa kutoka Maraban-Jos, ambayo inayofuata Abuja na Minna. Njia kuu inayopiytia mji huu inaitwa Barabara Ahmadu Bello. Majina mengi ya maeneo katika mji huu yametokana na majina ya zamani Masultani, emirs na mashujaa wa vita. Kaduna ina soko kubwa,lilioundwa hivi karibuni baada ya moto katikati mwa mwaka wa 1990.

Kuna uwanja wa mashindano mkubwa, takriban maili moja mviringo, ambapo ndani mnaKlabu ya polo ya Ahmadu Yakubuna Kalabu ya mamba Kadunapia vilabu vya mchezo wa raga viko ndani mwa uwanja huo. Kuna viwanja vya ndege mbili, moja ambayo ni Uwanja wa ndege Kaduna .

Ofisi kuu ya Kampuni ya huduma za ndege ya Chanchangiiko Kaduna. [4]

Njia za reli[hariri | hariri chanzo]

Mnamo Septemba, mwaka wa 2009, ujenzi wa tawi la reli hadi mji mkuu wa Abuja ulipitishwa [5]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Fletcher, Banister; Dan Cruickshank (1996). "Africa". Sir Banister Fletcher's a History of Architecture. Architectural Press. uk. 1466. ISBN 0750622679. 
  2. ""BBC News - Kaduna: Nigeria's religious flashpoint"". Iliwekwa mnamo 2007-04-06. 
  3. ""BBC News - Nigeria Buries Its Dead"". Iliwekwa mnamo 2009-02-07. 
  4. "Contacts." Chanchangi Airlines. Kuzunduliwa tarehe 19 Oktoba 2009.
  5. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-12-17. Iliwekwa mnamo 2009-12-22. 

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

10°31′N 7°26′E / 10.517°N 7.433°E / 10.517; 7.433