Jumanne
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jumanne ni siku ya tatu ya katika juma (wiki) ya siku saba yenye asili ya kiyahudi-kikristo. Iko kati ya siku za Jumatatu na Jumatano.
[hariri] Kiswahili, Kiarabu na utamaduni wa Kiislamu
Katika lugha ya Kiswahili jina la siku lina namba "4" ndani yake. Hii ni dokezo la asili ya Kiswahili katika utamaduni ya Kiislamu pasipo na athira ya Uyahudi unaoanza hesabu baada ya sikukuu ya Kiislamu ya Ijumaa ambayo ni siku ya sala ya pamoja: Jumamosi kama siku ya kwanza baada ya Ijumaa, Jumapili kama siku ya pili, Jumatatu kama siku ya tatu n.k.. Tabia hii katika Kiswahili ni ya pekee hasa kwa sababu Kiarabu ambacho ni lugha ya Korani takatifu na lugha ya kimataifa ya Waislamu kinafuata hesabu ya Kiyahudi na kuiita siku "ya tatu" (ثلاثاء - thalatha).
Lugha nyingi za nchi za Kiislamu zafuata kawaida ya Kiarabu na kuiita "siku ya tatu", kwa mfano Kiindonesia (selasa - tatu) au Kiajemi (Farsi) (سهشنب - se shanbe tatu jumamosi).
Katika lugha za Ulaya jina la siku hutunza kumbukumbu ya miungu iliyoabudiwa zamani za dini za Kiroma au Kigermanik kama vile Kifaransa "mardi" (siku ya Mars) au Kiingereza "Tuesday" (siku ya Tiu).
| Makala hiyo kuhusu "Jumanne" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Jumanne kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |
| Siku za juma (wiki) |
|---|
| Jumapili - Jumatatu - Jumanne - Jumatano - Alhamisi - Ijumaa - Jumamosi |
}