Juhudi za Msela

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
"Juhudi za Msela"
"Juhudi za Msela" kava
Wimbo wa Dknob

kutoka katika albamu ya Bomoa Mipango

Umetolewa 2004-2005
Umerekodiwa 2005
Aina ya wimbo Hip hop
Urefu 5:03
Studio Midman Records
Mtunzi Dknob
Mtayarishaji Jonas Kiwale
Bomoa Mipango orodha ya nyimbo
  1. Dakika Tatu
  2. Yupi ni Yupi - Akimsh. Benjamin
  3. Ingewezekana - Akimsh. Ray C na Squeezer
  4. Juhudi za Msela
  5. Dear Mtoto
  6. We Unasemaje - Akimsh. Benjamin
  7. Mfalme wa Mitaani - Akimsh. Only Face
  8. Kitu Gani - Akimsh. Q Jay
  9. We Unasemaje (rmx) - Akimsh. Benjamin
  10. Kitu Gani (rmx) - Akimsh. Q Jay

"Juhudi za Msela" ni jina la wimbo ulioimbwa na kutungwa na msanii wa hip hop kutoka nchini Tanzania, Dknob. Wimbo unatoka katika albamu Bomoa Mipango. Wimbo ulitayarishwa na Jonas Kiwile kupitia studio za Midaman Records. Wimbo ulitolewa kunako mwaka 2005.

Wimbo na mashairi[hariri | hariri chanzo]

Katika mashari yake anaanza kwa kusema:

Mstari wa kwanza

Sitaki mbichi hizi, nataka mbivu mtini. Ndiyo maana saa yangu iko mbele dakika kumi. Karibu sana backstage yangu viwanjani, para kichwani, bandara shingoni, albamu sokoni - nnabuku mfukoni.

Halafu anaiitikia kwa kuimba:

Hizi ni juhudi za masela hakuna kulemba tunatafuta hela, Toka asubuhi mpaka night! Ngoja-ngoja kwanza na-fight!

Kijana niko vitani risasi zangu ni pini nachenguja na mashiti, lakini simwabudu shetani. Kukaba mtu kweupe na kivuli chake ndiyo zake...

Katika wimbo huu, hasa anamzingumzia maisha ya kija asiye na kazi halafu anajaribu kujitafutia kwa hali na mali. Hata kama itakuwa kwa kukaba au kuiba, basi ilimradi yeye mkono uende kinywani. Anazungumzia maisha ya vijana waliowengi mtaani.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]