Juda Thadaeus Ruwa'ichi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Juda Thadeus Ruwa'ichi, O.F.M.Cap. ni askofu mkuu wa jimbo kuu la Kanisa Katoliki la Dar es Salaam, Tanzania.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa tarehe 30 Januari 1954 katika kijiji cha Legho Mulo, kata ya Kilema Kusini, Wilaya ya Moshi Vijijini, mkoa wa Kilimanjaro kama mwana parokia ya Mt. Bernadeta Kilema katika Jimbo Katoliki la Moshi.

Alijiunga na utawa wa Fransisko wa Asizi katika tawi la Ndugu Wadogo Wakapuchini.

Mwaka 1981 alipadrishwa akahudumu katika shirika lake la Kifransisko katika nyadhifa mbalimbali na katika nchi mbalimbali, hadi alipoteuliwa na Papa Yohane Paulo II kuwa askofu wa Mbulu mwaka 1999.

Mwaka 2005 alihamishwa kuwa askofu wa Dodoma na tangu Januari 2011 hadi Juni 2018 alikuwa askofu mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza.

Ndipo alipohamishwa tena kwenda jimbo kuu la Dar es Salaam kama mwandamizi wa kardinali Polycarp Pengo. Huyo alipostaafu tarehe 15 Agosti 2019, Ruwa'ichi akashika uongozi kamili wa jimbo kuu hilo.

Tangu mwaka 2006 alipata kuwa rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania hadi muda wake ulipokwisha (Julai 2012).

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.

Watu wengi wanamfahamu kama kiongozi wa wakatoliki wa Tanzania