Joyce Cherono Laboso

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Joyce Laboso

Dk. Joyce Cherono Laboso ni mwanasiasa wa Kenya na mbunge katika bunge la Kenya

Eneo Bunge[hariri | hariri chanzo]

Yeye anawakilisha Jimbo la uchaguzi la Sotik katika bunge la Kumi Alikichukua kiti hiki kutoka kwa dadake Lorna Laboso ambaye alifariki katika ajali ya ndege mnamo 10 Juni 2008.

Matokeo ya Uchaguzi Mdogo[hariri | hariri chanzo]

Katika Uchaguzi mdogo uliofanyika 25 Septemba,2008, Dk. laboso aliyekuwa akiwania kiti hicho kwa tiketi ya ODM, aliwabwaga wapinzani wengine 11 na kujinyakulia kura 23,880; ushindi wa zaidi ya kura 10,000 zaidi ya mpinzani wake wa karibu Alexander Sitienei aliyezoa kura 13,843.

Taaluma nyingine[hariri | hariri chanzo]

Kabla ya kuchaguliwa kuwa mbunge, Dk. Laboso alikuwa mkufunzi wa Lugha ya Kifaransa katika Chuo Kikuu cha Egerton. Sasa hii yeye pia ni Mwanakamati katika Kamati ya Kitaifa ya Jinsia na Maendeleo.[1]

Tazama Pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Joyce Cherono Laboso kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.