Joseph Smith, Kijana
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Joseph Smith, Kijana (23 Desemba 1805 - 27 Juni 1844) alikuwa mwanzilishi na kiongozi wa Wamormoni. Mwaka wa 1827 alidai kuwa malaika alimtokea na kufunulia maagizo ya Mungu katika kitabu kipya, yaani Kitabu cha Mormoni. Mwaka wa 1830 alikichapisha kitabu hicho. Miaka ya 1830, makao makuu ya Wamormoni yalianza jimboni Ohio, baadaye jimboni Missouri na kuanzia mwaka wa 1838 jimboni Illinois. Pale Smith Kijana alitawala kama mwenyekiti wa kijiji mpaka alipouawa na umati wa watu wasiokubali utawala wake. Alifuatwa kama kiongoi wa Wamormoni na Brigham Young aliyewaongoza Wamormoni kuhamia jimbo la Utah.
| Makala hii kuhusu mtu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Joseph Smith, Kijana kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |