John Cheruiyot Korir
John Cheruiyot Korir (alizaliwa Disemba13, 1981) ni mwanariadha wa Kenya ambaye hulishughulisha na mbio za masafa Marefu. Anajulikana kwa sifa yake ya kungara katika majaribio lakini kushindwa katika mashindano makubwa[1].
Yaliyomo |
Historia [hariri]
Korir alizaliwa katika mji wa Kiramwok, Wilaya ya Bomet nchini Kenya. alianza kukimbia akiwa katika shule ya Msingi. Alifuzu kutoka Shule ya Sekondari ya Merigi mnamo 1998. Hatimaye alisajiliwa na Kikosi cha Kenya Army mnamo 2001. Yeye ni wa kabila la Kipsigis, ambalo ni tabaka dogo la Kalenjin.
John Cheruiyot Kori na John Kipsang Korir [hariri]
John Cheruiyot Korir anafaa kutofautishwa kutoka kwa John Kipsang Korir ambaye sana sana hushiriki katika mashindano ya Amerika. Wawili hawa wameshindana mara kadhaa. Katika mashindano ya Lisbon Half Marathon ya 2002, Kipsang Korir aliibuka bora, huku Cheruiyot akimshinda Kipsang katika shindano la Cross Country nchini Kenya mnamo 2003.
Katika shindano la Cherry Blossom 10-Mile Run la 2005, John Cheruiyot Korir aliibuka wa tano katika huku John Kipsang Korir akilishinda shindano hilo[2][3].
Meneja na Kocha [hariri]
Meneja wake ni Gianni Demadonna, huku kocha wake akiwa Renato Canova.
Mafanikio [hariri]
Matokeo ya Kujivunia [hariri]
Uwanjani
- Mita 3000 7:43.35 (2000)
- Mita 5000 13:09.58 (2000)
- Mita 10,000 26:52.87 (2002)
Barabarani
- Kilomita 10 27:49 (2005)
- Kilomita 15 43:26 (2003)
- Half marathon 1:00:47 (2004)
Viungo vya Nje [hariri]
- IAAF wasifu wa John Cheruiyot Korir
- IAAF: Focus on athletes
Virejeleo [hariri]
- ↑ IAAF, 1 Desemba 2006 John Cheruiyot Korir, the favourite in Lagos - PREVIEW
- ↑ Cherry Blossom: 28 Machi 2005: Two John Korirs Meet; Sally Barsosio Favorite in Women's Race
- ↑ Cherry Blossom 10 Mile Road Race results 2005
- ↑ Matokeo ya Addis Ababa 2008