John Atta Mills

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
John Atta Mills


wa 3 Rais wa Ghana
(4th Republic)

wa 2 Makamu wa Rais wa Ghana
(4th Republic)
Muda wa Utawala
7 Januari 1997 – 7 Januari 2001

John Evans Atta Mills (amezaliwa 21 Julai 1944 )[1] ni Rais wa sasa wa Ghana. Alichaguliwa tarehe 7 Januari 2009, baada ya kumshinda mgombea wa chama tawala Nana Akufo-Addo kwa 50.23% -49.77% katika uchaguzi wa 2008 .[2] Alikuwa Makamu wa Rais 1997-2001 chini ya Rais Jerry Rawlings ,naye akasimama bila mafanikio katika uchaguzi wa rais wa mwaka 2000 na 2004 kama mgombea wa chama cha National Democratic Congress (NDC).

Maisha ya awali, elimu na taaluma ya kazi[hariri | hariri chanzo]

Mills alizaliwa katika Tarkwa, iliyoko katika Mkoa wa Magharibi wa Ghana.[1] Alielimishwa katika shule ya Achimota ,ambapo yeye alihitimu shahada yake mwaka 1963, na Chuo Kikuu cha Ghana, Legon, ambapo yeye alipewa shahada na cheti taalamu katika sheria mwaka 1967.

Wakati akisoma kiwango cha udaktari katika Sheria kutoka Shule ya Oriental and African Studies (SOAS) katika Chuo Kikuu cha London, Mills alikuwa amechaguliwa kwa ugenini, kama msomi wa Fulbright katika Chuo cha Sheria cha Stanford huko Marekani.[2][3]

Mills alihitimu masomo yake ya udaktari katika SOAS, baada ya kukamilisha makala yake ya Thesis katika eneo la ushuru na maendeleo ya kiuchumi. Kazi ya Mills rasmi ya kufunza ilikuwa kama mhadhili wa Kitivo cha Sheria katika Chuo Kikuu cha Ghana, Legon. Alikaa karibu miaka ishirini na mitano akifunza katika Legon na taasisi nyingine za elimu ya juu, na akapanda cheo kuanzia mhadhili, mhadhili mkuu na Profesa, na ni mjumbe katika bodi na kamati mbalimbali. Zaidi ya hayo, yeye alisafiri kutembelea duniani kote kama mhadhili na profesa katika taasisi ya elimu kama vile LSE, na kufafanua utafiti wake na majarida katika mikutano mbali mbali.[3]

Machapisho:[hariri | hariri chanzo]

Mills ametunga machapisho kadhaa, kama vile [3]

  • Taxation of Periodical or Deferred Payments arising from the Sale of Fixed Capital (1974)
  • Exemption of Dividends from Income taxation: A critical Appraisal (1977) Katika: Review of Ghana Law, 1997, 9: 1, pag.38-47
  • Report of the Tax Review Commission, Ghana, parts 1,2&3 (1977)
  • Ghana's Income Tax laws and the Investor. ( iliyochapishwa na Chuo Kikuu cha Ghana)
  • Ghana's new investment code : an appraisal (1993) Katika: University of Ghana Law Journal, 1993, vol. 18, pag.1-29

Yeye ameshikilia nafasi za mtahini katika taasisi kadhaa zenye uhusiano na fedha taasisi nchini Ghana, ikiwa ni pamoja na Taasisi ya Wahasibu, Taasisi ya wafanyikazi wa Benki, na Tume ya ushuru ya Ghana.[3]

Mchango katika michezo[hariri | hariri chanzo]

Amechangia katika shirika la Ghana la Hockey, Shirika la kitaifa la Michezo nchini, na klabu ya Accra Hearts of Oak. Yeye anafurahia Hockey na kuogelea ,na huchezea kwa mara timu ya taifa ya Hockey (yeye bado ni mwanachama wa timu ya Hockey Veterans).[3]

Urais[hariri | hariri chanzo]

Tarehe 21 Desemba 2006, Mills alichaguliwa na NDC kama mgombea wake kwa ajili ya uchaguzi wa rais wa 2008 kwa jumla ya 81.4% (kura 1,362), mbali akishinda wapinzani wake, Ekwow Spio-Garbrah, Alhaji Mahama Iddrisu, na Eddie Annan.[3][4] Mwaka 2008, alichaguliwa kuwa rais wa Ghana, baada ya uchaguzi wa pande tatu.

Shughuli na miradi mingine[hariri | hariri chanzo]

Mills amehusika katika shughuli na miradi mbalimbali kama vile [3]

  • Mwanachama wa soko la hisa la Ghana
  • Bodi ya Wadhamini, Mines Trust
  • Mjumbe wa Kamati ya usimamizi, Utawala wa ushuru ya Wataalam, Umoja wa Mataifa Kikundi cha Wataalam katika Ushirikiano wa Kimataifa katika Masuala ya ushuru, na Umoja wa Mataifa Mradi wa Sheria na Idadi ya Watu
  • Masomo juu kukodesha vifaa nchini Ghana
  • Kitabu kiandalizi juu ya ushuru ya Mapato ya Ghana
  • Mapitio ya Mkataba na Uingereza wa ushuru
  • Mwaka 1988, John Evans Atta Mills akawa kaimu Kamishna wa Mapato ya Ndani ya Humuma ya Ghana na aliteuliwa kamishna mwezi Septemba 1996.
  • Mwaka 1997, Profesa Mills alipata cheo kingine muhimu tarehe 7 Januari 1997, alipoapa kama Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Ghana.
  • Katika 2002, Prof Mills alikuwa kutembelea Liu kama msomi mtalii katika Kituo cha Masomo ya Maswala ya Dunia, Chuo Kikuu cha British Columbia, Kanada.
  • Mnamo Desemba 2002, John Evans Atta Mills alichaguliwa na chama chake kuwa kiongozi na akawaongoza katika uchaguzi wa 2004.

Maisha ya Kibinafsi.[hariri | hariri chanzo]

Rais wa Ghana, John Evans atta Mills, pamoja na Mchungaji TB Joshua

Ameoa Ernestina Naadu Mills, mkufunzi na ana mwana mwenya umri wa miaka 19, Sam Kofi Mills na Ruby Addo.

Alikuwa rafiki mzuri wa Mchungaji TB Joshua, The Synagogue, Kanisa la mataifa yote, mjini Lagos, na hutembelea kanisa lake mara kwa mara. Alisema kufuatia uzinduzi wake kwamba TB Joshua alitabiri kwamba kungekuwa na uchaguzi wa tatu, matokeo yangetolewa Januari, na angeweza kuibuka mshindi.[5][6][7]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 Profaili ya atta Mills, Archived 28 Septemba 2007 at the Wayback Machine. Ghanareview.com.
  2. 2.0 2.1 Kokutse, Francis. "Opposition leader wins presidency in Ghana", Associated Press, 2009-01-03. Retrieved on 2009-01-04. 
  3. 3.0 3.1 3.2 3.3 3.4 3.5 3.6 John Atta Mills & John Mahama - The Change We Deserve. National Democratic Congress. Jalada kutoka ya awali juu ya 2015-02-01. Iliwekwa mnamo 2009-01-25.
  4. "NDC CONGRESS RESULTS-Prof Wins", Modernghana.com, 22 Desemba 2006.
  5. Ateba, Simon. "‘T.B. Joshua Predicted My Victory’—Ghana’s Leader", PM News, 2009-01-12. Retrieved on 2009-12-23. Archived from the original on 2011-12-31. 
  6. Babalola, Ebun. "The Synagogue: When President Attah Mills Came Calling", Vanguard, 2009-01-20. [dead link]
  7. Adegbamigbe, Ademola. "Mill's Day At The Synagogue", The News, 2009-01-19. 

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]