Kito (madini)
Mandhari
(Elekezwa kutoka Johari 2)
Kito (pia: johari, jiwe la thamani) ni madini adimu na ngumu zinazopendeza kwa sababu ya uangavu na rangi yake. Vito mbalimbali vinapendwa na watu na kutumiwa kama mapambo. Kito chenye ugumu na thamani kubwa ni almasi.
Mara nyingi vinakatwa, kusuguliwa na kung'arishwa kwa namna mbalimbali na kutumiwa pamoja na metali adili kama dhahabu au fedha kuwa mapambo kama pete, hereni, mkufu au bizimu.
Mifano ya vito ni
Lulu na korali hutajwa wakati mwingine pia kama kito ingawa si minerali asilia lakini dutu inayotengenezwa na wanyama.
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kito (madini) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |