Johann Paul Schor

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mchoro wa jengo la Palazzo del Qirinale ambalo Johann alishiriki katika kulipamba
Mchoro wa jengo la Palazzo Borghese ambalo alishirikiana na Carlo Rainaldi kuunda sanamu ya chemichemi

Johann Paul Schor (1615 - 1674), anajulikana katika jiji la Roma kama "Giovanni Paolo Tedesco" (jina hili Tedesco linamaanisha Mjerumani katika Kiitaliano). Johann alikuwa msanii wa kutoka nchi ya Austria. Alikuwa mzalishaji wa michoro ya kupamba katika Baroque Roma, akichora michoro ya vitanda, milipuko ya mapambo,fedha ,nguo na hata mapambo ya vyakula vya sukari. Michoro yake mingi, hapo zamani, imehusishwa na Bernini.

[hariri] Wasifu

Alizaliwa katika eneo la Innsbruck akiwa mwana wa familia kubwa ya kisanaa ya Tyrolese. Alipokea mafunzo kutoka studio ya baba yake, Hans Schor. Katika mwaka wa 1640, yeye alijenga jina lake katika Roma. Hapo, katika mwaka wa 1654, akawa mwanachama wa Accademia di San Luca, shule ya ya wasanii.

Akifuatilia mifano ya Bernini na Pietro da Cortona, uzuri wa michoro yake ulimpa umaarufu miongoni mwa wasanii na wapenzi wa sanaa Hibbard (1958): "aliunda kazi yake kwa njia ya kisanaa ya Cortona na Bernini kwa uhuru ulioonekana kutokana na Callot na Stefano Della Bella na wakati mwingine huonekana kushinda rococo". Akiwa chini ya Cortona alisaidia katika kupamba Palazzo del Qirinale kwa ajili ya papa Alexander VII Chigi. Katika mwaka wa 1659, papa alimteua Schor katika kazi ya kutumia michoro ya Bernini katika ujenzi wa kanisa la familia ya Chigi ('Capella Della Madonna del Voto katika Duomo di Siena). Akiwa Roma,Schor alimsaidia Bernini katika kuunda kifaa cha kukifunika Kiti Cha Mtakatifu Petro (Lanciani 1892) na katika kazi nyinginezo katika mwisho wa miaka ya 1650s na 1660s. (Hibbar 1958:205 noti ya 10). Labda kazi yake maarufu kabisa ilikuwa baldaccino huko Santo Spirito huko Sassia.

Schor pia alisaidia kupamba vyumba vya Vatikano na katika Palazzo Borghese, aliposhirikiana na Carlo Rainaldi katika kupamba chemichemi ya nympheum iliyokuwa ikionyesha Venus akioga. Hapo baadaye aliandaa michoro ya kupendekeza miundo mipya ya kupamba dari katika Palazzo Colonna (1665-1668).

Upungufu wake kama msanii unaweza kuonekana kwa pambo alilounda la Musurgia Universalis,1650 ya Athanasius Kircher [1] lakini pambo hilo liliharibika kwa mipango mingi aliyotaka Kircher. Alipokuwa akifanya kazi pekee yake, michoro yake ilionyesha kazi bora zaidi.[2]

Katika studio yake katika miaka ya 1670 alimwajiri msanii wa Austria aliyekuwa kijana bado, Johann Bernhard Fischer. Fischer alirudi Vienna na akafanya kazi yake hadi akapewa taji la Fischer Von Erlach, msanii maarufu wa asili ya Kivienna aliyefuzu katika miundo ya Baroque.

Johann Paulo Schor alikufa huko Roma katika mwaka wa 1674.

Wana wake Schor, Giovanni Paolo na Fillipo waliendeleza studio yake baada ya kifo chake. Wote wawili walikuwa miongoni mwa wasanii wa Roma waliopolekwa Naples na kiongozi Gasparo de Haro y Guzman, marqués del Carpio,katika mwaka wa 1683. Miongoni mwa wanamuziki wa kiongozi huyo alikuwa Alessandro Scarlatti. Del Carpio alikutana na wasanii hawa kwa kupitia mwana wa mfalme Lorenzo Onofrio Colonna,aliyekuwa mwanajeshi wa Naples ilhali del Cprio alikuwa balozi wa Kihispania.[3] Katika mwaka wa 1690,Cristofor Schor alifanya mabadiliko madogo kwa muundo wa Martino Longhi wa Sant'Antonio dei Portoghesi. Johann Ferdinand Schor alikuwa msaidizi wa studio wa Carlo Maratta.

[hariri] Maelezo

  1. ^ Howard Hibbard, "Palazzo Borghese Studies I: The Garden and Its Fountains" Gzaeti la Burlington 100 No. 663 (Juni 1958, pp. 204–212,)

[hariri] Marejeo

Vifaa binafsi
Maeneo ya wiki

Vibadala
Vitendo
Urambazaji
Vifaa
Lugha zingine