Jimbo la Uchaguzi la Siakago
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Siakago ni Jimbo la Uchaguzi nchini Kenya. Ni moja kati ya majimbo mawili yaliyo katika Wilaya ya Mbeere. Jimbo hili lina wodi tano na zote huwachagua madiwani kwa baraza la Mbeere County. Mji wa Siakago ambao ni mji mkuu wa Wilaya ya Mbeere unapatikana katika kata ya Nthawa katika jimbo hili.
Yaliyomo |
Historia [hariri]
Jimbo hili lilianzishwa wakati wa uchaguzi mkuu wa 1988 wakati jimbo kuu la Embu Mashariki liligawanwa kutengeneza Jimbo la Runyenjes na Siakago.
Silvester Mate, Mbunge wa kwanza wa Siakago, ndiye alikuwa pia mbunge wa mwisho wa Embu Mashariki baada ya kushinda kiti hicho wakati wa Uchaguzi Mkuu a 1983[1].
Wabunge [hariri]
| Uchaguzi | Mbunge [1] | Chama | Vidokezo |
|---|---|---|---|
| 1988 | Silvester Mate | KANU | Mfumo wa Chama Kimoja |
| 1992 | Gerald Ireri Ndwiga | KNC | Ndwiga alihamuia KANU mnamo 1995 na kushinda uchaguzi mdogo uliofuatia |
| 1997 | Silas M’Njamiu Ita | DP | Ita aliaga dunia mnamo 1999 [2] |
| 1999 | Justin Bedan Njoka Muturi | KANU | Uchaguzi Mdogo |
| 2002 | Justin Bedan Njoka Muturi | NARC | |
| 2007 | Kivuti Maxwell | Safina |
Kata na Wodi [hariri]
| Kata | |
| Kata | Idadi ya Watu* |
|---|---|
| Gituburi | 8,005 |
| Ishiara | 13,575 |
| Kanyuambora | 11,658 |
| Kiangombe | 8,294 |
| Muminji | 8,390 |
| Mutitu | 7,040 |
| Ndurumori | 9,750 |
| Nthawa | 16,892 |
| Jumla | x |
| *Hesabu ya 1999 [3]. | |
| Wodi | |
| Wodi | Wapiga Kura Waliojisajili |
|---|---|
| Ishiara | 4,685 |
| Kanyuambora | 4,812 |
| Kiang'ombe | 6,844 |
| Muminji | 5,883 |
| Nthawa | 9,808 |
| Jumla | 32,032 |
| *Septemba 2005 [4]. | |
Tazama Pia [hariri]
- Jimbo la Uchaguzi la Runyenjes
- Maeneo bunge ya Kenya
- Uchaguzi Mkuu wa Kenya, 2007
- Uchaguzi Mkuu wa Kenya, 2002
- Uchaguzi Mkuu wa Kenya, 1997
- Uchaguzi Mkuu wa Kenya, 1992
Virejeleo [hariri]
- ↑ 1.0 1.1 Center for Multiparty Democracy: Politics and Parliamenterians in Kenya 1944-2007
- ↑ Daily Nation, 22 Aprili 1999: Siakago MP dies in hospital
- ↑ information.go.ke: CDF allocation by sector and location (2003-6)
- ↑ Electoral Commission of Kenya: Registered voters per polling station by electoral area/ward and constituency
Viungo vya Nje [hariri]