Jimbo kuu la Songea
Jimbo kuu la Songea (kwa Kilatini Archidioecesis Songeana) ni mojawapo kati ya majimbo makuu 5 ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania, likiongoza majimbo ya kusini, yakiwemo Mbinga, Tunduru-Masasi, Mtwara, Lindi, Mbeya, Njombe na Iringa.
Makao makuu ni mjini Songea, ambapo pana Kanisa kuu la mtakatifu Mathias Mulumba Kalemba.
Askofu mkuu ni Norbert Wendelin Mtega.
Yaliyomo |
Takwimu (mwaka 2004) [hariri]
Jimbo lenyewe la Songea lina waamini 223.111 (46.9%) kati ya wakazi 476.161 wa eneo lote la kilometa mraba 38,600.
Mapadri ni 105, ambao kati yao 62 ni wanajimbo na 43 watawa. Hivyo kwa wastani kila mmojawao anahudumia Wakatoliki 2,124 katika parokia 27.
Pia jimboni wanaishi mabruda 227 na masista 458.
Historia [hariri]
Baada ya hatua mbalimbali ya uinjilishaji chini ya wamonaki Wabenedikto, tarehe 6 Februari 1969 jimbo liliundwa rasmi, halafu tarehe 18 Novemba 1987 lilifanywa jimbo kuu kwa hati Christi Domini ya Papa Yohane Paulo II.
Maaskofu [hariri]
- Willibrord Lay, O.S.B. † (1913 - 1922)
- Gallus (Bernhard) Steiger, O.S.B. † (22 Februari 1922 - 6 Desemba 1952 kujiuzulu)
- Eberhard (Hermann) Spiess, O.S.B. † (23 Septemba 1953 - 6 Februari 1969 kujiuzulu)
- James Joseph Komba † (6 Februari 1969 - 1 Februari 1992)
- Norbert Wendelin Mtega, tangu 6 Julai 1992
Viungo vya nje [hariri]
- [www.catholic-hierarchy.org ukurasa [1]
- (Kiingereza) [2] katika tovuti ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania
- Hati Non sine magna, AAS 20 (1928),uk. 97
- Hati Ex orientali parte, AAS 24 (1932),uk. 262
- Hati Christi Domini
- (Kiingereza) Scheda dell'arcidiocesi su www.gcatholic.com