Jimbo katoliki la Mahenge
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jimbo katoliki la Mahenge (kwa Kilatini Dioecesis Mahengensis) ni mojawapo kati ya majimbo ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania na kama hayo yote linafuata mapokeo ya Roma.
Makao makuu yake yako Mahenge katika mkoa wa Morogoro.
Kikanisa linahusiana na jimbo kuu la Dar-es-Salaam.
Askofu wake ni Agapiti Ndorobo.
Yaliyomo |
Historia[hariri]
- 21 Aprili 1964: Kuanzishwa kama Dayosisi ya Mahenge kutokana na jimbo kuu la Dar-es-Salaam
- 2012: Maeneo ya Jimbo Katoliki la Ifakara yalitengwa na jimbo la Mahenge
Maaskofu[hariri]
-
- Agapiti Ndorobo (tangu 1995.03.03)
- Patrick Iteka (1973.06.14 – 1993.08.22)
- Nikasius Kipengele (1970.06.25 – 1971.12.07)
- Elias Mchonde (1964.04.21 – 1969.06.13)
Takwimu[hariri]
Eneo ni la kilometa mraba 39,498, ambapo kati ya wakazi 531,237 (2004) Wakatoliki ni 465,696 (97.7%).