Jimbo katoliki la Iringa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Jimbo katoliki la Iringa (kwa Kilatini Dioecesis Iringaënsis) ni mojawapo kati ya majimbo 33 ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania na kama hayo yote linafuata mapokeo ya Kiroma.

Makao makuu yake yako Iringa katika mkoa wa Iringa, lakini linaenea pia katika mkoa wa Mbeya.

Kanisa kuu limewekwa wakfu kwa Moyo Mtakatifu wa Yesu.

Kikanisa linahusiana na jimbo kuu la Songea kuanzia tarehe 18 Novemba 1987.

Askofu wake ni Tarcisius Ngalalekumtwa.

Parokia ni 33.

Anwani ya posta ni: P.O. Box 133, Iringa, Tanzania.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Uongozi[hariri | hariri chanzo]

Takwimu[hariri | hariri chanzo]

Eneo ni la kilometa mraba 43,318, ambapo kati ya wakazi 2,367,962 (2006) Wakatoliki ni 588,438 (24.9%). Mapadri ni 92, wakiwemo wanajimbo 53 na watawa 39. Kwa wastani kila mmoja anahudumia waamini 6.396. Shemasi ni 1, mabruda ni 206 na masista 549.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]