Jimbo Katoliki la Mbeya
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jimbo katoliki la Mbeya (kwa Kilatini Dioecesis Mbeyaënsis) ni mojawapo kati ya majimbo 33 ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania na kama hayo yote linafuata mapokeo ya Kiroma.
Kikanisa linahusiana na jimbo kuu la Songea.
Askofu wake ni Evaristo Marc Chengula.
Yaliyomo |
Historia [hariri]
- 1932: Kuanzishwa kwa Apostolic Prefecture ya Mbeya kutokana na Apostolic Vicariate ya Tanganjika
- 1949: Kupandishwa cheo kuwa Apostolic Vicariate ya Mbeya
- 25 Machi 1953: Kufanywa dayosisi
Uongozi [hariri]
- Maaskofu wa Mbeya
- Evaristo Marc Chengula (since 1996)
- James Dominic Sangu (1966 – 1996)
- Antoon van Oorschoot MAfr (1953 – 1964)
- Vicar Apostolic wa Mbeya
- Antoon van Oorschoot MAfr (1949 – 1953)
- Prefect Apostolic wa Mbeya
- Antoon van Oorschoot MAfr (1947 – 1949)
- Ludwig Haag MAfr (1938 – 1947)
- Max Theodor Franz Donders MAfr (1932 – 1938)
Takwimu [hariri]
Eneo ni la kilometa mraba 60,348, ambapo kati ya wakazi 2,082,000 (2006) Wakatoliki ni 347,347 (16.7%).