Jihadi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Jihadi (Ar. ‏جهاد‎ jihād) ni neno lenye asili ya Kiarabu lenye maana ya kujitahidi kwa ajili ya Allah katika dini ya Uislamu.

Jihadi kati ya Waislamu wa leo[hariri | hariri chanzo]

Leo hii ina maana tatu kati ya Waislamu hasa

  1. kutetea imani ya kiislamu pamoja na kulinda umma ya Waislamu, pia kutetea Waislamu wanaoshambuliwa.
  2. kushindana na udhaifu wa nafsi na kujitahidi kuwa mtu mwema
  3. jitihada za kuboresha umma ya Waislamu.[1]

Waislamu kadhaa wanaitumia pia kwa maana ya kueneza Uislamu hata kwa njia ya silaha na matishio. Hapa kuna hata vikundi kama Al Qaida wanaotumia mbinu za ugaidi kwa jihadi jinsi wanavyoielewa. Ingawa idadi yao si kubwa kati ya Waislamu kwa jumla watu wengi nje ya Uislamu wanaelewa neno hasa kwa maana inayotangazwa na hao.

Jihadi katika Qurani[hariri | hariri chanzo]

Katika Qurani neno jihadi liko mara 41 mara nyingi katika msemi "jihadi kwenye njia ya Mungu (الجهاد في سبيل الله al-jihad fi sabil Allah)".[2][3][4] . Katika Qurani "jihadi" huwa hasa na maana ya kijeshi lakini si wazi kama ni [5]. Si wazi kama maana hii ilikuwa mapigano dhidi ya wenye imani tofauti kwa jumla au vita ya kitetezi tu. Mtu anayehusika katika jihadi huitwa "mujahid". Jihadi ni wajibu wa kidini kwa Waislamu.

Jihadi katika mafundisho ya wataalamu wa shari'a[hariri | hariri chanzo]

Katika mafundisho wa wataalamu Waislamu wa karne za kwanza baada ya Muhammad jihadi hii ilikuwa na shabaha ya kupanusha eneo chini ya utawala wa Uislamu na utetezi wake, hadi Uislamu ungekuwa dini tawala.[6] Hii haikuwa na shabaha kuwalazimisha wote wasiokuwa Waislamu kupokea dini hii. Katika mafundisho ya wataalamu wa kale wale walioitwa "wapagani" walipaswa kushambuliwa hadi wakubali Uislamu au wauawe. Lakini watu wa "ahl al-kitab" yaani wenye misahafu yaani Wakristo, Wayahudi na Wasabayi walipewa nafasi ya kukubali kipaumbele cha Waislamu na kuishi chini ya utawala wa Waislamu katika hali ya dhimma. Katika mwendo wa upanuzi wa utawala wa Kiislamu nafasi ya dhimma iliongezwa pia kwa dini nyingine kama Uzoroasta na Uhindu ingawa hao wana na miungu mingi sana. Mwishoni karibu kila jumuiya ya kidini ilipewa nafasi ya kukubali hali ya dhimma. [7]

Maelezo[hariri | hariri chanzo]

  1. Jihad. BBC (2009-08-03).
  2. Morgan, Diane (2010). Essential Islam: a comprehensive guide to belief and practice. ABC-CLIO, 263. ISBN 0313360251. Retrieved on 5 Januari 2011. 
  3. Wendy Doniger, ed (1999). Merriam-Webster's Encyclopedia of World Religions. Merriam-Webster. ISBN 087-7790442. , Jihad, p.571
  4. Josef W. Meri, ed (2005). Medieval Islamic Civilization: An Encyclopedia. Routledge. ISBN 041-5966906. , Jihad, p.419
  5. Rudolph Peters: Jihad in Classical and Modern Islam. Markus Wiener Publishing Inc., 2005. S. 2. Vgl. Fred M. Donner: The Sources of Islamic Conceptions of War. In: John Kelsay und James Turner Johnson (ed.): Just War and Jihad: Historical and Theoretical Perspectives on War and Peace in Western and Islamic Traditions. Greenwood Press, 1991. S. 47
  6. Linganisha: The Encyclopaedia of Islam. New Edition. Brill, Leiden. Bd. 2, S. 538 („Djihad“): „In law, according to general doctrine and in historical tradition, the djihād consists of military action with the object of the expansion of Islam and, if need be, of its defence.“
  7. Robert Hoyland (Hrsg.): Muslims and Others in Early Islamic Society. Ashgate, 2004. p. xiv.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]