Jeromu Emilian
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mtakatifu Jeromu Emiliani (1486 – 8 Februari, 1537) alikuwa padri na mtawa nchini Italia.
Ametambuliwa na Kanisa Katoliki kuwa mtakatifu na msimamizi wa mayatima.
Sikukuu yake ni tarehe 8 Februari.
Yaliyomo |
[hariri] Maisha
Jeromu Emiliani alizaliwa mjini Venisi huko Italia mwaka 1486.
Kwanza alikuwa askari, lakini baadaye akaacha kazi hiyo ili ajitoe mhanga kuwahudumia maskini; akawapa mali yake yote.
Baada ya kupata upadri (1518) alianzisha Utawa wa Makleri ulioitwa Wasomaska, ili kuwasaidia mayatima na maskini.
Alikufa mwaka 1537 huko Somasca, karibu na mji wa Bergamo.
[hariri] Tazama pia
[hariri] Marejeo
- "Sala ya Kanisa - Vipindi vya Liturjia", Toleo la Tatu 1996, Ndanda - Peramiho: Benedictine Publications, uk.1283
[hariri] Viungo vya nje
- St. Jerome Emiliani. Catholic Encyclopedia.
- Sanamu yake kama mwanzilishi katika Basilika la Mt. Petro (Vatikani).
| Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jeromu Emilian kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
