Jamhuri ya Masedonia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Република Македонија
Republika Makedonija

Jamhuri ya Masedonia
Bendera ya Jamhuri ya Masedonia Nembo ya Jamhuri ya Masedonia
Bendera Nembo
Wito la taifa: {{{national_motto}}}
Wimbo wa taifa: Денес над Македонија
Leo juu ya Masedonia
Lokeshen ya Jamhuri ya Masedonia
Mji mkuu Skopje (tamka: "skopye"
42°0′ N 21°26′ E
Mji mkubwa nchini Skopje
Lugha rasmi Kimasedonia1
Serikali Parliamentary Jamhuri
Branko Crvenkovski
Nikola Gruevski
Independence
Ilitangazwa
8 Septemba 1991
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
25,333 km² (ya 148)
1.9
Idadi ya watu
 - 2005 kadirio
 - Msongamano wa watu
 
2,034,000 (ya 143)
79/km² (ya 110)
Fedha Denar ya Masedonia (MKD)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
CET (UTC+1)
CEST (UTC+2)
Intaneti TLD .mk
Kodi ya simu +389

-

1Kimasedonia ni lugha rasmi ya kwanza. Kialbania ni lugha rasmi ya pili pamoja na Kimasedonia; kila lugha inayotumiwa na 20% ya wakazi hutumiwa kama lugha rasmi ya nyongeza kimahal kama vile Kituruki, Kiserbia, Kiromany na Kiaromania.


Ramani ya Jamhuri ya Masedonia

Jamhuri ya Masedonia (Република Македонија / Republika Makedonija) ni nchi kwenye rasi ya Balkani katika Ulaya ya kusini mashariki. Imepakana na Serbia, Albania, Ugiriki na Bulgaria. Jina rasmi la kimataifa ni "Masedonia iliyokuwa jamhuri ya Yugoslavia" (tazama chini).

Mji mkuu ni Skopje yenye wakazi 600,000. Miji midogo zaidi ni pamoja na Bitola, Prilep, Tetovo, Kumanovo, Ohrid, Veles, Štip, Gostivar na Strumica.

Masedonia ni nchi mwanachama ya Umoja wa Mataifa na inasubiri kupokelewa katika Umoja wa Ulaya.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Masedonia ya Kale[hariri | hariri chanzo]

Katika karne kabla ya Kristo Masedonia iliuwa eneo katika kaskazini ya Ugiriki. Wakazi wake wanaaminiwa walisema lahaja za Kigiriki lakini mara nyingi hawakutambuliwa na Wagiriki wenyewe kama wenzao jinsi tunavyojua kutoka waandishi wa Ugiriki ya Kale. Manmo 500 KK kulikuwako ufalme uloitwa Masedonia na wafalme waliruhusiwa kwenye michezo ya Olimpiki ya madola ya Wagiriki.

Pamoja na sehemu nyingi za Ugiriki ufalme huu ulipaswa kukubali ubwana wa Milki ya Uajemi lakini mfalme Filipo alifaulu kuanzia mnamo mwaka 360 KK kurudisha uhuru wa ufalme akaendelea kuifanya Masedonia kuwa dola kiongozi kati ya madola madogo ya Ugiriki. Mwanawe Aleksander aliimarisha utawala wake juu ya Wagiriki wengine na kushambulia Milki ya Uajemi na kuivamia na kushinda kwa jeshi la Wagiriki kutoka sehemu zote. Mnamo mwaka 3225 mfalme wa Masedonia alitawala nchi zote kuanzia Ugiriki hadi Misri, Syria, Ujamei, mipaka ya Uhindini na Asia ya Kati.

Baada ya kifo cha Aleksander mnamo 323 KK milki yake iligawiwa na Masedonia ilikuwa tena ufalme wa pekee. Ikaendelea kwa kujitegema hadi uenezaji wa Dola la Roma ikawa jimbo la Kiroma tangu mwaka 147 KK. Baadaye ufalme wa awali iligawiwa kwa majimbo mbalimbali. Wakazi walibadilika polepole kutokana na uhamiaji ndani ya Dola la Roma.

Kufika kwa Waslavoni[hariri | hariri chanzo]

Tangu karne ya 6 BK makabila ya Waslavoni yalifika katika sehemu zilizowahi kuitwa Masedonia zamani. Sehemu kubwa za eneo ilikuwa chini ya milki ya Wabulgaria, tangu 1018 sehemu ya jimbo la Bulgaria katika Milki ya Bizanti. Mnamo 1392 Waturuki Waosmani walianza kuvamia Masedonia iliyoendelea kukaa chini ya Milki ya Osmani hadi 1912.

Masedonia ya kisasa[hariri | hariri chanzo]

Sehemu kubwa za Masedonia ya Kale leo hii ziko ndani ya Ugiriki na pia Bulgaria. Jamhuri ya leo ina tabia ya pekee kwa sababu ilikuwa sehemu ya Yugoslavia hadi 1991. Masedonia ni eneo linalokaliwa hasa na Waslavoni wanaozungumzwa lugha iliyo karibu na Kibulgaria na Kiserbia. Eneo hili lilitawaliwa kwa muda mrefu na Dola la Uturuki. Si rahisi kujua watu wa sehemu hizi walianza lini kujisikia kama watu tofauti na wa pekee na majirani yao hasa Wabulgaria. Inaonekana hii ilitokea hasa wakati wa karne ya 20.

Masedonia ya leo ilikuwa jimbo la kujitawala la Yugoslavia. Baada ya mwisho wa shirikisho la Yugoslavia Masedonia nayo ilitafuta uhuru wake. Mwanzoni palikuwa na matatizo ya kutumia jina kwa sababu ya upinzani wa Bulgaria na Ugiriki zinazodai kuwa "Masedonia" ni sehemu ya urithi wao wa kitaifa. Kwa muda nchi ilijulikana rasmi kama "Masedonia iliyokuwa jamhuri la Yugoslavia" lakini yenyewe inajiita "Jamhuri ya Masedonia".

Wakazi na utamaduni[hariri | hariri chanzo]

Wamasedonia waslavoni ni takriban theluthi mbili za wakazi wote. Robo moja ni Waalbania. Wengine ni mchanganyiko wa vikundi vidogovidogo kama Waturuki, Waromany, Waserbia na Wabosnia.

Wamasedonia wenyewe ni hasa Wakristo Waorthodoksi. Waalbania ni hasa Waislamu. Lakini zaidi ya theluthi ya watu wote husema ya kwamba hawana dini. Hii inaaminiwa ni urithi wa kipindi cha ukomunisti nchini.

Europa Mapa.png Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Jamhuri ya Masedonia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.