Jamhuri ya Kituruki ya Kupro ya Kaskazini

Kutoka Wikipedia

Kupro ya Kaskazini
Kupro ya Kaskazini

Jamhuri ya Kituruki ya Kupro ya Kaskazini (Kituruki: Kuzey Kıbrıs Türk Cumhuriyeti) iko sehemu ya kaskazini ya kisiwa cha Kupro. Eneo lake ni 3,335 km² kuna wakazi lakhi mbili karibu wote ni Waturuki pamoja na Wagiriki 3,000 waliobaki kwenye rasi ya Rizokarpaso. Mji mkuu ni sehemu ya kituruki ya Nikosia.

Ni eneo lililojitenga na Jamhuri ya Kupro baada ya vita ya 1974. Hadi wakati ule Wakupro Wagiriki (waliokuwa wengi) na Wakupro Waturuki (waliokuwa takriban robo ya wakazi) waliishi pamoja pande zote za kisiwa. 1974 maafisa Wagiriki wa jeshi la Kupro walipindua serikali ya Askofu Makarios kwa shabaha ya kuunganisha kisiwa na Ugiriki. Uturuki uliingia kati ukavamia kisiwa kwa kusudi ya kukinga wakazi wenyeji Waturuki.

Waturuki walitwaa theluthi ya kaskazini ya kisiwa. Wakupro Wagiriki 160,000 kutoka kaskazini walikimbia kwenda kusini na Waturuki 50,000 kutoka kusini wakakimbia kaskazini.

Hata baada ya mwisho wa uasi na kurudi kwa rais Askofu Makarios jeshi la Uturuki likakataa kundoka tena. 1973 Dola la Kujitawala la Kituruki la Kupro likatangazwa. 1983 Jamhuri ya Kituruki ya Kupro ya Kaskazini ikatangaza uhuru wake lakini haikutambuliwa na UM wala na nchi yoyote isipokuwa Uturuki.

Wakupro Waturuki walio wengi wameondoka kisiwani wakihamia Uingereza na nchi nyingine. Idadi kubwa ya watu wenye utamaduni wa Kituruki kisiwani wamehamia kutoka Uturuki bara baada ya uvamizi wa jeshi la Uturuki.

[hariri] Viungo vya Nje


Nchi na maeneo ya Ulaya
Albania | Andorra | Austria | Belarus | Bosnia na Herzegovina | Bulgaria | Kroatia | Denmark | Eire | Estonia | Ufaransa | Hungaria | Iceland | Italia | Jamhuri ya Masedonia | Latvia | Liechtenstein | Lithuania | Luxemburg | Malta | Moldova | Monako |Montenegro | Norway | Poland | Romania | San Marino | Serbia3 | Slovakia | Slovenia | Hispania | Ubelgiji | Uceki | Ufini | Ugiriki | Ujerumani | Uholanzi | Ureno | Urusi1 | Uswidi | Uswisi | Ukraine | Uingereza | Vatikani

Maeneo ya Ulaya ya kujitawala chini ya nchi nyingine: Visiwa vya Faroe | Gibraltar | Guernsey | Jan Mayen | Jersey | Isle of Man | Svalbard

Nchi za Asia ambazo ni mwanachama wa baraza la Ulaya au vyombo vingine vya Ulaya: Armenia2 | Azerbaijan1 || Cyprus2 | Georgia1 | Kazakhstan1 | Uturuki1

Nchi zisizokubaliwa na umma wa kimataifa: Abkhazia | Nagorno-Karabakh2 | Ossetia ya Kusini | Transnistria | Jamhuri ya Kituruki ya Kupro ya Kaskazini2

Maelezo: (1) nchi ya kimabara katika Asia na Ulaya; (2) nchi katika eneo la Asia ya Magharibi (kufuatana na kanda za UM) lakini kiutamaduni huhesabiwa kuwa sehemu ya Ulaya; (3) Inaelekea kugawiwa kuwa nchi mbili za Serbia na Montenegro

Image:WikiLettreMini.png Makala hiyo kuhusu "Jamhuri ya Kituruki ya Kupro ya Kaskazini" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri".

Ikiwepo makala kuhusu Jamhuri ya Kituruki ya Kupro ya Kaskazini kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili.

Vifaa binafsi