Jacques Monod
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jacques Lucien Monod (9 Februari, 1910 – 31 Mei, 1976) alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Ufaransa. Hasa alichunguza usanisi wa vimeng'enya ndani ya chembe hai. Mwaka wa 1965, pamoja na Francois Jacob na Andre Lwoff alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.

