Italia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Itali)
Rukia: urambazaji, tafuta
Repubblica Italiana
Jamhuri ya Italia
Bendera ya Italia Nembo la Italia
Lugha rasmi Kiitalia; kijimbo pia Kijerumani, Kifaransa, Kiladino, Kislovenia, Kisardinia
Mji Mkuu Roma
Rais Giorgio Napolitano
Waziri Mkuu Enrico Letta
Eneo 301.338 km²
Wakazi 60.494.632 (31-7-2010) (23º duniani)
Wakazi kwa km² 198.8
JPT 31,022 US-$ (2008)
Pesa Euro
Wakati UTC+1
Wimbo wa Taifa Fratelli d'Italia (Ndugu wa Italia)
Sikukuu ya Jamhuri 2. Juni
Sikukuu ya Taifa 25. Aprili
Simu ya kimataifa +39
Italia katika Ulaya na katikati ya Bahari ya Kati.
Ramani ya Italia
Italia jinsi inavyoonekana kutoka angani

Jamhuri ya Italia ni nchi ya Ulaya Kusini. Eneo lake ni 301.338 km² ambalo lina wakazi 60.494.632 (31-7-2010) (ni nchi ya 23 duniani kwa wingi wa watu). Wengi wao ni Wakristo wa Kanisa Katoliki.

Yaliyomo

Jiografia [hariri]

Umbo lake linafanana na mguu linalozungukwa na maji ya Mediteraneo pande tatu. Visiwa viwili vikubwa vya Sicilia na Sardinia ni sehemu za Italia pamoja na visiwa vidogovidogo.

Imepakana na Ufaransa, Uswisi, Austria na Slovenia.

Nchi mbili ndogo zinazozungukwa na eneo la Italia ni San Marino na Vatikano.

Historia [hariri]

Peninsula ya Italia iliunganishwa mara ya kwanza na Jamhuri ya Roma (509-27 K.K.), lakini hiyo ilipoenea Ulaya, Afrika ya Kaskazini na Asia ya Magharibi ikawa na sura ya kimataifa.

Umoja ulipotea kuanzia uvamizi wa Roma (476) na hasa baada ya ufalme wa Karolo Mkuu.

Juhudi za kuurudisha zilifanywa hasa katika karne ya 19, ambapo Ufalme wa Sardinia ulitekwa sehemu kubwa ya Italia (hasa miaka 1860, 1866 na 1870).

Baada ya vita vikuu vya pili iligeuka Jamhuri yenye katiba inayotia mamlaka kuu mikononi mwa bunge.

Ni kati ya nchi sita zilizoanzisha Umoja wa Ulaya mwaka 1957 ikaendelea kuunga mkono ustawi wake hadi uanzishaji wa pesa la pamoja (Euro).

Maendeleo [hariri]

Italia ni nchi iliyoendelea, ikiwa na nafasi ya saba kwa nguvu ya kiuchumi duniani, hivyo ni mwanachama wa G7, G8 na G20.

Pia ni nchi inayongoza duniani kwa kuwa na mahali pengi (45) pa kimaumbile na pa kihistoria palipoingizwa katika orodha ya UNESCO ya "Urithi wa Dunia".

Viungo vyo nje [hariri]

Tazama pia [hariri]


Nchi za Umoja wa Ulaya Bendera ya Umoja wa Ulaya
Austria | Bulgaria | Denmark | Estonia | Finland | Hungaria | Ireland | Italia | Kupro | Latvia | Lituanya | Luxemburg | Malta | Poland | Slovakia | Slovenia | Hispania | Romania | Sweden | Ubelgiji | Uceki | Ufaransa | Ugiriki | Uholanzi | Uingereza| Ujerumani | Ureno
Italy looking like the flag.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Italia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Italia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.