Israeli (maana)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Israeli ni jina linalotaja

  • Nchi ya Israeli ya kisasa
  • Israeli ya Kale ambayo ni nchi au pia jumuiya ya watu ambao historia yao husimuliwa katika Biblia.
  • Watu wa Biblia wanaotajwa katika Tanakh au Agano la Kale na pia Agano Jipya
    • Yakubu mwana wa Isaka mwana wa Ibrahimu (Abrahamu) alipewa jina la Israeli baada ya ushindani wake na Mungu (tazama Mwanzo (Biblia) 32,29 "maana umeshindana na Mungu na watu nawe umeshinda"
    • jina la pamoja kwa ajili ya makabila 12 waliotokana na wana 12 wa Yakobo-Israeli, mara nyingi kwa umbo la Wanaisraeli
    • jina la milki ya kaskazini ya Israeli (milki) iliyoanzishwa baada ya kifo cha mfalme Suleimani kando la milki ya Yuda; historia yao kwa jumla hujadiliwa chini ya jina "Israeli ya Kale".
    • Baada ya angamizi la milki ya kaskazini katika vita dhidi ya Ashuri jina lilitumiwa kwa ajili ya watu wa milki ya kusini yaani watu wa milki ya Yuda
    • Baada ya angamizi la milki hii ya kusini jina lilitaja Wayahudi kama jumuiya ya kidini na taifa lililokaa katika sehemu mbalimbali (linganisha matumizi katika Agano jipya kwenye Waraka kwa Waroma 9,6 na 11,25)
      • Kwa kutaja Wayahudi jina latumiwa katika Qurani mara nyingi kama "wana wa Israeli"
    • Kwa watu wanaoitwa taifa teule katika Tanakh au Agano la Kale tazama kwa jumla Israeli ya Kale


  • Israeli ni pia jina la kawaida kati ya Wayahudi hadi leo