Isimujamii
Isimujamii (pia isimu jamii) ni tawi la isimu ambalo huchunguza uhusiano kati ya lugha na jamii. Aidha inajihusisha na athira yeyote ya jamii kama vile desturi za watu, matazamio, na muktadha, katika nyanja za lugha namna inavyotumika. Neno hili kwa Kiingereza huitwa: Sociolinguistics.
Chini ya taaluma hiyo, kuna matawi mengi yanayoshughulikia uchanganuzi wa vipengele fulani vya uhusiano kati ya lugha na jamii, k.m.
- uhusiano kati ya lugha na utamaduni
- matumizi ya aina tofauti za lugha na mazingira yake, kama lahaja, rejista na mtindo
- matumizi ya lugha tofauti wakati mmoja, kama katika wingilugha, ubadilishaji msimbo na diglosia
- vipengele mbalimbali vya mawasiliano kupitia maoni ya msemaji (tawi hilo pia huitwa isimu amali)
- matumizi ya lugha baina ya jamii za watu tofauti, kama lugha mawasiliano, pijini na krioli
- uhusiano kati ya lugha na siasa katika upangaji lugha na sera za lugha
Marejeo [hariri]
- TUKI 1990, "Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha", Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
- Massamba, David 2004, "Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha", Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
- Buliba, Aswani, Kimani Njogu & Alice Mwihaki 2006, "Isimujamii kwa Wanafunzi wa Kiswahili", Nairobi: The Jomo Kenyatta Foundation
macha kutokka sauti ana kubali maelezo haya kwani ni vitu viwili vinavyoambatana
Viungo vya Nje [hariri]
- Applied Linguistics Resources on Dmoz (Kiingereza)
Tazama pia [hariri]
Viambishi ni mofimu au viungo vyenye maana ambavyo hufungamanishwa na mzizi/shina la neno ili kulipa neno hilo maana mbalimbali za kisarufi kama vile nafsi, wakati, hali, urejeshi, n.k Viambishi awali ni vile vinavyotangulia mzizi wenyewe, yaani huwa kabla ya mzizi/shina. SHINA AU MZIZI: Hakuna tofauti kati ya shina na mzizi MZIZI/SHINA, Ni sehemu ya neno inayobeba maana yake kuu na huwa haibadiliki, Kwa mfano, tuangalie vitenzi vifuatavyo: a-na-LIM-a wa-li-LIM-i-a ni-ta-LIM-iw-a wa-na-vyo-LIM-a Ukiangalia kwa makini, utaona kuna sehemu ya kitenzi hiki ambayo haibadiliki katika mifano ya hapo juu. Sehemu hiyo ni (-LIM-). Na hii ndiyo shina au mzizi wa kitenzi LIMA. Mfano mwingine: a-li-ki-SOM-a hu-SOM-ew-a wa-li-SOM-e-an-a a-li-m-SOM-e-a i-li-SOM-w-a Tunaona hapa mzizi/shina la kitenzi SOMA, ni -som- Ili utambue shina/mzizi wa kitenzi unafaa kuwazia hali mbalimbali au kauli tofautitofauti za mnyambuliko wa kitenzi halafu ubainishe sehemu isiyobadilika.