Ipsilon
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Ipsiloni)
| Alfabeti ya Kigiriki | |||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|
| Herufi za kawaida | |||||||
| Α α Alfa | 1 | Ν ν Ni | 50 | ||||
| Β β Beta | 2 | Ξ ξ Ksi | 60 | ||||
| Γ γ Gamma | 3 | Ο ο Omikron | 70 | ||||
| Δ δ Delta | 4 | Π π Pi | 80 | ||||
| Ε ε Epsilon | 5 | Ρ ρ Rho | 100 | ||||
| Ζ ζ Dzeta | 7 | Σ σ ς Sigma | 200 | ||||
| Η η Eta | 8 | Τ τ Tau | 300 | ||||
| Θ θ Theta | 9 | Υ υ Ipsilon | 400 | ||||
| Ι ι Iota | 10 | Φ φ Phi | 500 | ||||
| Κ κ Kappa | 20 | Χ χ Khi | 600 | ||||
| Λλ Lambda | 30 | Ψ ψ Psi | 700 | ||||
| Μ μ Mi | 40 | Ω ω Omega | 800 | ||||
| Herufi za kihistoria1 | |||||||
| 6 | 90 | ||||||
| 6 | 90 | ||||||
| 8 | 90 | ||||||
| 900 |
|
||||||
| 1 Viungo vya Nje: Alfabeti_ya_Kigiriki#Viungo_vya_Nje |
|||||||
Ipsilon (pia: Ypsilon au kigiriki Ύψιλον "i fupi") ni herufi ya 20 katika alfabeti ya Kigiriki ikawa baadaye herufi ya 25 katika alfabeti ya Kilatini. Iliandikwwa kama Y ya Kiswahili lakini ilikuwa vokali si konsonanti.
Katika Kigiriki cha Kale ilitaja pia namba 400.
Waroma waliipokea mara mbili katika alfabeti ya Kilatini:
- mwanzoni katika karne za KK kupitia Kietruski kwa umbo la V lililomaanisha mara sauti ya "u" mara ya "w/v".
- baada ya kuenea kwa utawala wao hadi Ugiriki katika karne ya 1 KK na kupokea maneno mengi ya Kigiriki.
Ipsilon ya kigiriki ilitaja vokali iliyokuwa kati ya "u" na "i" (kama Kijerumani "ü"); katika Kigiriki cha kisasa ni "i" pekee.
Asili yake ilikuwa Waw ya Kifinisia.