Indi
Kutoka Wikipedia
| Indi (Indium) |
|
|---|---|
|
|
|
| Jina la Elementi | Indi (Indium) |
| Alama | In |
| Namba atomia | 49 |
| Mfululizo safu | Metali |
| Uzani atomia | 114.818 |
| Valensi | 2, 8, 18, 18, 3 |
| Densiti | 7.31 g/cm³ |
| Kiwango cha kuyeyuka | 429.75 K (156.60 °C) |
| Kiwango cha kuchemka | 2345 K (2072 °C) |
| Asilimia za ganda la dunia | 1 · 10-5 % |
| Hali maada | mango |
| Mengineyo | Isotopi ya kawaida ina kiwango kidogi cha unururifu |
Indi ni elementi. Namba atomia yake ni 49 kwenye mfumo radidia na uzani atomia ni 114.818. Jina limepatikana kutoka kwa rangi ya indigo au buluu ya Kihindi katika taswirangi yake.
Ni metali haba na laini yenye rangi ya kifedha-nyeupe.
Hupatikana hasa katika mitapo za zinki.
Indi ina matumizi mengi ila tu kutokana na uhaba wake hutumiwa zaidi katika kampaundi si metali tupu. Siku hizi sehemu kubwa hutumiwa kwa umbo la oksidi ya indi katika skrini nyembamba za kompyuta na televisheni. Matumizi mengine ni ya kilainishaji ndani ya mashine.
| Makala hiyo kuhusu "Indi" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Indi kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |

